د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

د مخ نمبر:close

external-link copy
36 : 6

۞ إِنَّمَا يَسۡتَجِيبُ ٱلَّذِينَ يَسۡمَعُونَۘ وَٱلۡمَوۡتَىٰ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ ثُمَّ إِلَيۡهِ يُرۡجَعُونَ

Hakika wale wanaokukubali wewe, ewe Mtume, kwa yale unayoyalingania ya uongofu ni wale ambao wanayasikia maneno kwa kuyakubali. Ama makafiri, wao wamo kwenye hesabu ya wafu. Kwani uhai wa kikweli unakuwa kwa Uislamu. Na wafu, Mwenyezi Mungu Atawatoa kutoka kwenye makaburi yao wakiwa hai. Kisha watarudi Kwake Siku ya Kiyama ili watimiziwe hesabu yao na malipo yao. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 6

وَقَالُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يُنَزِّلَ ءَايَةٗ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na washirikina walisema, kwa ujeuri na kiburi, «Kwa nini Mwenyezi Mungu Hateremshi alama iyoneshayo ukweli wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, miongoni mwa alama za kimiujiza.» Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwateremshia miujiza, lakini wengi wao hawajui kwamba kuteremsha miujiza kunakuwa kulingana na hekima Yake, Aliyetukuka.» info
التفاسير:

external-link copy
38 : 6

وَمَا مِن دَآبَّةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا طَٰٓئِرٖ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِي ٱلۡكِتَٰبِ مِن شَيۡءٖۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ يُحۡشَرُونَ

Hakuna katika ardhi mnyama yoyote anayetembea chini au ndege anayepaa juu kwa mbawa zake isipokuwa ni aina ya makundi yaliyoumbwa kama nyinyi. Hatukuacha katika Allawh, Almaḥfūd (Ubao Uliohifadhiwa) chochote isiopokuwa tumekithibitisha. Kisha wao, Siku ya Kiyama, watafufuliwa wapelekwe kwa Mola wao, na hapo Mwenyezi Mungu Atamhesabu kila mtu kwa alilolitenda. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 6

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا صُمّٞ وَبُكۡمٞ فِي ٱلظُّلُمَٰتِۗ مَن يَشَإِ ٱللَّهُ يُضۡلِلۡهُ وَمَن يَشَأۡ يَجۡعَلۡهُ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na wale waliozikanusha hoja za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni viziwi hawasikii yanayowafaa, ni mabubu hawaitamki haki. Wao wametunduwaa kwenye giza, hawakufuata njia iliyolingana sawa. Yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumpoteza Anampoteza na yule Anayetaka kumuongoza Anamfanya awe kwenye njia iliyolingana sawa. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 6

قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ أَوۡ أَتَتۡكُمُ ٱلسَّاعَةُ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَدۡعُونَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Nipeni habari, ikiwajia adhabu ya Mwenyezi Mungu ulimwenguni, au ikawajia saa ya nyinyi kufufuliwa, je, mutamuomba hapo asiyekuwa Mwenyezi Mungu awaondolee shida iliyowakumba, iwapo nyinyi ni wakweli kwamba waungu wenu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wanawanufaisha au kuwadhuru?» info
التفاسير:

external-link copy
41 : 6

بَلۡ إِيَّاهُ تَدۡعُونَ فَيَكۡشِفُ مَا تَدۡعُونَ إِلَيۡهِ إِن شَآءَ وَتَنسَوۡنَ مَا تُشۡرِكُونَ

Bali hapo mtamuomba Mola wenu Aliyewaumba, si mwingine, na mtamtaka Awaokoe na Awaondolee shida kubwa zilizowashukia Akitaka, kwani Yeye Ndiye Muweza wa kila kitu; na wakati huo mtaacha masanamu wenu na wategemewa wenu. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 6

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَأَخَذۡنَٰهُم بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَتَضَرَّعُونَ

Hakika tuliwatuma, ewe Mtume, Wajumbe kuwaendea makundi ya watu kabla yako kuwalingania kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wakawakanusha na tukawapa mtihani katika mali yao, kwa ufukara mwingi na dhiki za maisha, na tukawapa mitihani katika miili yao, kwa magonjwa na kuumwa, ili wajidhalilishe kwa Mola wao na wanyenyekee Kwake Peke Yake kwa ibada. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 6

فَلَوۡلَآ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَا تَضَرَّعُواْ وَلَٰكِن قَسَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Basi si ilipowajia, umma hawa wenye kukanusha, mitihani yetu wajidhalilishe kwetu. Lakini wao nyoyo zao zilisusuwaa na Shetani aliwapambia yale ambayo waliokuwa wakiyafanya ya maasia na wakiyaleta ya ushirikina. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 6

فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِۦ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِمۡ أَبۡوَٰبَ كُلِّ شَيۡءٍ حَتَّىٰٓ إِذَا فَرِحُواْ بِمَآ أُوتُوٓاْ أَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ فَإِذَا هُم مُّبۡلِسُونَ

Basi walipoacha kufuata amri za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kuzipa mgongo, tuliwafungulia milango ya kila kitu miongoni mwa riziki, ndipo tukawabadilishia shida kwa kuwapa raha ya maisha, na tukawabadilishia magonjwa kwa kuwapa uzima wa miili, kwa kuwavuta kidogo kidogo. Hata watakapofanya kiburi na wakajiona kwa mema na neema tulizowapa, tutawashushia adhabu ya ghafla, wakitahamaki watajikuta wamekata tamaa wamekatika na kila zuri. info
التفاسير: