د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

Al-Hadid

external-link copy
1 : 57

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Vinamtakasa Mwenyezi Mungu viumbe Vyake vyote vilivyoko mbinguni na ardhini. Na Yeye ni Mshindi juu ya viumbe Vyake, Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo yao. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 57

لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ni Yake mamlaka ya mbinguni na ardhini na vilivyomo ndani yake. Yeye Ndiye Mmiliki Mwenye kuendesha mambo ya viumbe Vyake, Anahuisha na kufisha, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna kinachomshinda Akikitaka kifanyike, Anachokitaka kinakuwa, na Asichokitaka hakiwi. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 57

هُوَ ٱلۡأَوَّلُ وَٱلۡأٓخِرُ وَٱلظَّٰهِرُ وَٱلۡبَاطِنُۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ

Yeye Ndiye wa Mwanzo Ambaye hakukuwa na chochote kabla Yake, na Ndiye wa Mwisho Ambaye hakuna kitu chochote baada Yake, na Ndiye Aliyejitokeza Ambaye hakuna kitu chochote juu Yake, na Ndiye wa ndani Ambaye hakuna kitu chochote kilicho karibu kuliko Yeye, na hakuna chochote kinachofichamana Kwake ardhini wala mbinguni, na Yeye ni Mjuzi wa kila kitu. info
التفاسير: