د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

د مخ نمبر:close

external-link copy
141 : 4

ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمۡ فَإِن كَانَ لَكُمۡ فَتۡحٞ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡ وَإِن كَانَ لِلۡكَٰفِرِينَ نَصِيبٞ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَسۡتَحۡوِذۡ عَلَيۡكُمۡ وَنَمۡنَعۡكُم مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلًا

Wanafiki ndio wale wanaongojea yatakayowashukia nyinyi, enyi Waumini, ya misukosuko na vita. Iwapo Mwenyezi Mungu Amewaneemesha kwa fadhila Zake, Akawanusuru juu ya adui yenu na mkapata ngawira, wao wanasema, «Kwani hatukuwa na nyinyi tukiwasaidia?» Na iwapo wakanushaji wa Dini hii wamepata sehemu ya ushindi na ngawira, wao wanasema kuwaambia, «Kwani hatukuwasaidia nyinyi kwa kile tulichowapatia na kuwahami na Waumini?» Basi Mwenyezi Mungu Ataamua baina yao na nyinyi Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu Hatawapa makafiri njia ya kuwashinda waja Wake wema. Basi mwisho mwema ni wa wacha- Mungu, duniani na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
142 : 4

إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَٰدِعُهُمۡ وَإِذَا قَامُوٓاْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُواْ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلٗا

Hakika mbinu ya wanafiki hawa ni kumhadaa Mwenyezi Mungu kwa Imani wanaojionyesha nayo na ukafiri wanaouficha, kwa kudhani kuwa mbinu yao itafichamana kwa Mwenyezi Mungu, na hali ni kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Anayewahadaa na ni Mwenye kuwalipa malipo yanayofanana na vitendo vyao. Wanafiki hawa wanaposimama kutekeleza Swala, wanasimama kufanya hivyo kwa uvivu, wanakusudia, kwa kuswali kwao, kuonekena na kusikika. Na wao hawamtaji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, isipokuwa kumtaja kwa uchache. info
التفاسير:

external-link copy
143 : 4

مُّذَبۡذَبِينَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ لَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِ وَلَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا

Hali ya hawa wanafiki ni kutokuwa na msimamo, kuchangayikiwa na kubabaika, hawathibiti kwenye hali moja, hawako pamoja na Waumini wala hawako pamoja na makafiri. Na yoyote ambaye Mwenyezi Mungu Ameupotoa moyo wake usimuamini na usishikamane na uongofu Wake, huyo hutampatia njia ya kufikia uongofu na yakini. info
التفاسير:

external-link copy
144 : 4

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ عَلَيۡكُمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينًا

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mkafuata sheria Yake! Msiwapende na kuwategemea wenye kukanusha Dini ya Mwenyezi Mungu na mkaacha kuwapenda kuwategemea Waumini na kuwapenda. Je, mnataka kwa kuwapenda maadui wenu kumpa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, hoja iliyo wazi kuwa nyinyi si wakweli katika Imani yenu? info
التفاسير:

external-link copy
145 : 4

إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِي ٱلدَّرۡكِ ٱلۡأَسۡفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمۡ نَصِيرًا

Hakika wanafiki watakuwa kwenye mahandaki ya chini kwa chini ya Moto Siku ya Kiyama. Na hutawapatia wao, ewe Mtume, yoyote wa kuwaokoa atakayewakinga wao wasifikie mwisho huu mbaya. info
التفاسير:

external-link copy
146 : 4

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَٱعۡتَصَمُواْ بِٱللَّهِ وَأَخۡلَصُواْ دِينَهُمۡ لِلَّهِ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَسَوۡفَ يُؤۡتِ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Isipokuwa wale ambao walirejea kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wakatubia Kwake, wakazirekebisha hali zao zilizoharibika za ndani na za nje, wakawategemea waja Wake Waumini, wakashikamana na dini ya Mwenyezi Mungu na wakamtakasia Yeye, Aliyetakasika kutokana na kila sifa ya upungufu. Hao ni pamoja na Waumini duniani na Akhera; na Mwenyezi Mungu Atawapa Waumini malipo kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
147 : 4

مَّا يَفۡعَلُ ٱللَّهُ بِعَذَابِكُمۡ إِن شَكَرۡتُمۡ وَءَامَنتُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ شَاكِرًا عَلِيمٗا

Mwenyezi Mungu hatawapa adhabu iwapo nyinyi mumefanya amali njema na mumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kwani Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Hana haja na yoyote asiyekuwa Yeye. Yeye Atawaadhibu waja kwa makosa yao. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarudishia shukrani[1] waja Wake kwa utiifu wao Kwake, ni Mjuzi wa kila kitu. info

[1]Maana ya Shākir ikinasibishwa na Mwenyezi Mungu ni «Analipa thawabu nyingi kwa mema machache». Ang. Tafsiri ya Ibn Kathīr Sura:2, aya:158.

التفاسير: