د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

external-link copy
6 : 22

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡحَقُّ وَأَنَّهُۥ يُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَأَنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Hayo yaliyotangulia kutajwa, miongoni mwa alama za uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, ndani yake pana dalili ya kukata kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kutakasika, Ndiye Mola Mwenye kuabudiwa kwa haki Ambaye hakuna anayefaa kuabudiwa isipokuwa Yeye, na Yeye Ndiye Mwenye kuwahuisha wafu, na Yeye ni Muweza wa kila kitu. info
التفاسير: