د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

external-link copy
80 : 2

وَقَالُواْ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامٗا مَّعۡدُودَةٗۚ قُلۡ أَتَّخَذۡتُمۡ عِندَ ٱللَّهِ عَهۡدٗا فَلَن يُخۡلِفَ ٱللَّهُ عَهۡدَهُۥٓۖ أَمۡ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Walisema Wana wa Israili, “Moto hautupati huko Akhera isipokuwa kwa siku chache zinazohesabika.” Waambie, ewe Mtume, kwa kuyavunja madai yao, “Kwani nyinyi muna ahadi, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ya jambo hilo? Mwenyezi Mungu Haendi kinyume ahadi yake. Lakini nyinyi munasema kuhusu Mwenyezi Mungu msiyoyajua kwa kuzua kwenu urongo.” info
التفاسير: