د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

external-link copy
186 : 2

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌۖ أُجِيبُ دَعۡوَةَ ٱلدَّاعِ إِذَا دَعَانِۖ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لِي وَلۡيُؤۡمِنُواْ بِي لَعَلَّهُمۡ يَرۡشُدُونَ

Na watakapo kukuuliza, ewe Nabii, waja Wangu kuhusu Mimi, waambie, «Mimi Niko karibu na wao, Nasikia maombi ya muombaji yoyote anaponiomba.Basi, ni wanitii Mimi katika Niliowaamrisha nayo na Niliowakaza nayo na waniamini Mimi, wapate kuongokewa kwenye maslahi yao ya dini yao na dunia yao. Katika ayah ii pana utoaji habari kutoka Kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, kuhusu ukaribu Wake kwa waja Wake, ukaribu unaolingana na utukufu Wake. info
التفاسير: