د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

external-link copy
84 : 16

وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ

Na wakumbushe, ewe Mtume, yale yatakayokuwa Siku ya Kiyama, tutakapowaletea kila kundi la watu Mtume wao akitolea ushahidi Imani ya walioamini miongoni mwao na ukanushaji wa wenye kukanusha. Kisha hao waliokanusha hawatapewa nafasi ya kuomba msamaha kwa waliyoyafanya, na hawatatakiwa kumridhisha Mola wao kwa kutubia na kufanya matendo mema, kwani wakati wa hilo ushapita. info
التفاسير: