د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

Al-Kauthar

external-link copy
1 : 108

إِنَّآ أَعۡطَيۡنَٰكَ ٱلۡكَوۡثَرَ

Sisi tumekupa, ewe Nabii, kheri nyingi za dunia na Akhera, miongoni mwazo ni mto wa Kauthar ulioko Peponi ambao pambizo zake ni mahema ya lulu na mchanga wake ni miski. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 108

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنۡحَرۡ

Basi, mtakasie Mola wako ibada yako yote na uchinje mnyama wako kwa ajili Yake, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 108

إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ ٱلۡأَبۡتَرُ

Mwenye kukutukia wewe na kuyatukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru ndiye itakayokatika athari yake na yeye mwenyewe kukatiwa kila kheri. info
التفاسير: