ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߊߥߊ߯ߤߟߌߞߊ߲ ߘߟߊߡߌ߬ߘߊ - ߙߎ߬ߥߊ߯ߘߎ-ߕߊ߬ߙߑߖߡߊ ߝߊ߲ߓߊ ߓߟߏ߫

ߞߐߜߍ ߝߙߍߕߍ:close

external-link copy
26 : 8

وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ أَنتُمۡ قَلِيلٞ مُّسۡتَضۡعَفُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ تَخَافُونَ أَن يَتَخَطَّفَكُمُ ٱلنَّاسُ فَـَٔاوَىٰكُمۡ وَأَيَّدَكُم بِنَصۡرِهِۦ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Na kumbukeni mlipokuwa wachache, mkidhoofishwa katika ardhi, mkiogopa kwamba watu watawanyakua, naye akawapa pahali pazuri pa kukaa, na akawaunga mkono kwa nusura yake, na akawaruzuku katika vilivyo vizuri ili mshukuru. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَخُونُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ وَتَخُونُوٓاْ أَمَٰنَٰتِكُمۡ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Enyi mlioamini! Msimhini Mwenyezi Mungu na Mtume, na mkahini amana zenu, hali ya kuwa mnajua. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 8

وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَأَوۡلَٰدُكُمۡ فِتۡنَةٞ وَأَنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni mtihani, na kwamba Mwenyezi Mungu ana ujira mkubwa kwake. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَتَّقُواْ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّكُمۡ فُرۡقَانٗا وَيُكَفِّرۡ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atawapa kipambanuo, na atawasitiria mabaya yenu,na awafutie dhambi, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 8

وَإِذۡ يَمۡكُرُ بِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيُثۡبِتُوكَ أَوۡ يَقۡتُلُوكَ أَوۡ يُخۡرِجُوكَۚ وَيَمۡكُرُونَ وَيَمۡكُرُ ٱللَّهُۖ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلۡمَٰكِرِينَ

Na walipokupangia vitimbi wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe. Na wakapanga vitimbi vyao, naye Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi vyake. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa wapangao vitimbi. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 8

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا قَالُواْ قَدۡ سَمِعۡنَا لَوۡ نَشَآءُ لَقُلۡنَا مِثۡلَ هَٰذَآ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّآ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na wanaposomewa Aya zetu, wao husema: Hakika tumesikia. Lau tungetaka, tungesema mfano wa haya. Haya si chochote isipokuwa ngano za wa mwanzo. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 8

وَإِذۡ قَالُواْ ٱللَّهُمَّ إِن كَانَ هَٰذَا هُوَ ٱلۡحَقَّ مِنۡ عِندِكَ فَأَمۡطِرۡ عَلَيۡنَا حِجَارَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ أَوِ ٱئۡتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٖ

Na waliposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tujie na adhabu yoyote iliyo chungu. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 8

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمۡ وَأَنتَ فِيهِمۡۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَهُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ

Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa uko miongoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba kusitiriwa dhambi. info
التفاسير: