[1] Hakuna hata mmoja katika Watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo) ambaye hatamwamini Isa, amani iwe juu yake, baada ya kuteremka kwake katika mwisho wa zama na kabla ya kufa kwake Isa katika zama hizo. Na Siku ya Kiyama, Isa, amani iwe juu yake, atakuwa shahidi juu ya matendo yao. Yale yanayokubaliana na sheria na yale yanayopingana nayo. (Tafsir Assa'adiy)