ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߊߥߊ߯ߤߟߌߞߊ߲ ߘߟߊߡߌ߬ߘߊ - ߙߎ߬ߥߊ߯ߘߎ-ߕߊ߬ߙߑߖߡߊ ߝߊ߲ߓߊ ߓߟߏ߫

external-link copy
258 : 2

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِي حَآجَّ إِبۡرَٰهِـۧمَ فِي رَبِّهِۦٓ أَنۡ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ إِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّيَ ٱلَّذِي يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۠ أُحۡيِۦ وَأُمِيتُۖ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأۡتِي بِٱلشَّمۡسِ مِنَ ٱلۡمَشۡرِقِ فَأۡتِ بِهَا مِنَ ٱلۡمَغۡرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِي كَفَرَۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Kwani hukumuona yule aliyehojiana na Ibrahim kuhusu Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim aliposema: Mola wangu Mlezi ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia ninahuisha na ninafisha. Ibrahim akasema: Kwa hakika, Mwenyezi Mungu hulileta jua kutokea mashariki, basi wewe lilete kutokea magharibi. Kwa hivyo, akashindwa yule aliyekufuru.[1] Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu dhalimu. info

[1] Alishindwa kwa hoja, kwa fikira, pia kwa ilimu na ufahamu.

التفاسير: