ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߊߥߊ߯ߤߟߌߞߊ߲ ߘߟߊߡߌ߬ߘߊ - ߙߎ߬ߥߊ߯ߘߎ-ߕߊ߬ߙߑߖߡߊ ߝߊ߲ߓߊ ߓߟߏ߫

ߞߐߜߍ ߝߙߍߕߍ:close

external-link copy
15 : 10

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَاتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا ٱئۡتِ بِقُرۡءَانٍ غَيۡرِ هَٰذَآ أَوۡ بَدِّلۡهُۚ قُلۡ مَا يَكُونُ لِيٓ أَنۡ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلۡقَآيِٕ نَفۡسِيٓۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۖ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana na Sisi husema, “Leta Qur-aani isiyokuwa hii, au ibadilishe.” Sema, “Haiwi kwangu niibadilishe nitakavyo mimi mwenyewe. Mimi sifuati isipokuwa yale ninayofunuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi ninahofu, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 10

قُل لَّوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوۡتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَدۡرَىٰكُم بِهِۦۖ فَقَدۡ لَبِثۡتُ فِيكُمۡ عُمُرٗا مِّن قَبۡلِهِۦٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Sema, “Mwenyezi Mungu angelitaka, nisingeliwasomea, wala nisingelikuwa mwenye kukijua zaidi yenu. Kwani nalikwisha kaa miongoni mwenu umri mzima kabla yake! Kwani, hamtii akilini?” info
التفاسير:

external-link copy
17 : 10

فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu na akazikadhibisha Ishara zake? Hakika hawafaulu wahalifu. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 10

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡ وَيَقُولُونَ هَٰٓؤُلَآءِ شُفَعَٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِۚ قُلۡ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Nao, wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema, “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!” Sema, “Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.” info
التفاسير:

external-link copy
19 : 10

وَمَا كَانَ ٱلنَّاسُ إِلَّآ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ فَٱخۡتَلَفُواْۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡ فِيمَا فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na watu hawakuwa isipokuwa Umma mmoja tu, kisha wakahitalifiana. Na lau kuwa si neno lililokwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingelikwisha katwa baina yao katika yale wanayohitalifiana. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 10

وَيَقُولُونَ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۖ فَقُلۡ إِنَّمَا ٱلۡغَيۡبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Na wanasema, “Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?” Sema, “Hakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.” info
التفاسير: