ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߥߊߤߟߌ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߊ߳ߺߊ߬ߟߌ߯ ߡߎߤ߭ߑߛߌߣߎ߫ ߊ.ߟߑߓߊߙߎ߯ߣߌ߮ ߓߟߏ߫

external-link copy
10 : 28

وَأَصۡبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَٰرِغًاۖ إِن كَادَتۡ لَتُبۡدِي بِهِۦ لَوۡلَآ أَن رَّبَطۡنَا عَلَىٰ قَلۡبِهَا لِتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingeli kuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini. info

Na mama yake Musa akawa hajitambui kwa dhiki iliyo muingia kwa kuwa mwanawe kaangukia mikononi mwa Firauni. Akawa anakurubia kujitambulisha kwamba yeye ndiye mama yake. Lau ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakuutia imara moyo wake kwa kusubiri, basi angeli tangaza kuwa huyo ni mwanawe, jinsi alivyo kuwa akimhurumia, na pia ili awe miongoni mwa Waumini wenye kutulia.

التفاسير: