ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߥߊߤߟߌ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߊ߳ߺߊ߬ߟߌ߯ ߡߎߤ߭ߑߛߌߣߎ߫ ߊ.ߟߑߓߊߙߎ߯ߣߌ߮ ߓߟߏ߫

external-link copy
58 : 2

وَإِذۡ قُلۡنَا ٱدۡخُلُواْ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةَ فَكُلُواْ مِنۡهَا حَيۡثُ شِئۡتُمۡ رَغَدٗا وَٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُولُواْ حِطَّةٞ نَّغۡفِرۡ لَكُمۡ خَطَٰيَٰكُمۡۚ وَسَنَزِيدُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na tulipo sema: Ingieni mji huu, na humo mle mpendapo maridhawa, na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, na semeni: Tusamehe! Tutakusameheni makosa yenu, na tutawazidishia wema wafanyao wema. info

Na kumbukeni enyi Wana wa Israili! Tulipo kwambieni: Ingieni katika mji mkubwa aliyo kutajieni Nabii wenu Musa na mle katika viliomo humo kama mnacho kitaka, kwa wingi na kwa wasaa, kwa sharti lakini kuwe kuingia kwenu kwa upole na unyenyekevu, kupitia mlango aliyo utaja Nabii wenu. Na kwamba hapo mumuombe Mwenyezi Mungu akusameheni makosa yenu. Kwani mwenye kufanya hayo kwa ikhlasi, usafi wa niya, tunamfutia makosa yake. Na mwenye kuwa mtenda mema aliye mt'iifu tunamzidishia thawabu na ukarimu juu ya kumsamehe na kumfutia dhambi.

التفاسير: