ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߊߥߊ߯ߤߟߌߞߊ߲ ߘߟߊߡߌ߬ߘߊ - ߊ߳ߺߓߑߘߎ-ߟߟߊ߯ߤߌ߫ ߡߎ߬ߤߊߡߡߊߘߎ߫ ߣߌ߫ ߣߊ߯ߛ߫ߌߙߎ߫ ߞ߭ߊ߬ߡߌ߯ߛߎ߫ ߓߟߏ߫

ߞߐߜߍ ߝߙߍߕߍ:close

external-link copy
7 : 9

كَيۡفَ يَكُونُ لِلۡمُشۡرِكِينَ عَهۡدٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ رَسُولِهِۦٓ إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّمۡ عِندَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ فَمَا ٱسۡتَقَٰمُواْ لَكُمۡ فَٱسۡتَقِيمُواْ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَّقِينَ

Haitakikani kwa washirikina wawe na makubaliano, mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, isipokuwa wale mliofanya makubaliano nao kwenye msikiti wa Ḥarām katika mapatano ya Hudaibiyah. Basi wakiendelea kutekeleza makubaliano yenu, na nyinyi endeleeni na wao kama hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda wenye kumuogopa Mwenyezi Mungu, wenye kutekeleza ahadi zao. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 9

كَيۡفَ وَإِن يَظۡهَرُواْ عَلَيۡكُمۡ لَا يَرۡقُبُواْ فِيكُمۡ إِلّٗا وَلَا ذِمَّةٗۚ يُرۡضُونَكُم بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَتَأۡبَىٰ قُلُوبُهُمۡ وَأَكۡثَرُهُمۡ فَٰسِقُونَ

Tabia ya Makafiri ni kujilazimisha na makubaliano iwapo ushindi uko kwa wengine wasiokuwa wao. Lakini wakijihisi kuwa wana nguvu juu ya Waumini, basi wao hawachungi ujamaa wala makubaliano. Basi msidanganyike na vile wanavyowafanyia wawapo na kicho na nyinyi. Kwani wao wanawaambia maneno kwa ndimi zao ili mridhike na wao, lakini nyoyo zao zinakataa hilo. Na wengi wao ni wenye kuupiga vita Uislamu, ni wenye kuvunja ahadi. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 9

ٱشۡتَرَوۡاْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلٗا فَصَدُّواْ عَن سَبِيلِهِۦٓۚ إِنَّهُمۡ سَآءَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Wameziacha aya za Mwenyezi Mungu na wakachukua badala yake vitu vya kilimwengu vilivyo duni, wakaipa mgongo haki na wakawazuia wale wanaotaka kuingia kwenye Uislamu wasiingie. Ni jambo ovu walilolifanya na ni kitendo cha kuchukiza walichokitenda. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 9

لَا يَرۡقُبُونَ فِي مُؤۡمِنٍ إِلّٗا وَلَا ذِمَّةٗۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُعۡتَدُونَ

Washirikina hawa wako kwenye vita dhidi ya Imani na watu wake, hawauekei uzito wowote ujamaa wa Muumini wala mapatano yake; walilonalo wao ni uadui na udhalimu. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 9

فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ فَإِخۡوَٰنُكُمۡ فِي ٱلدِّينِۗ وَنُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Na iwapo watakomeka na ibada ya asiyekuwa Mwenyezi mungu, wakalitamka neno la kumpwekesha, wakajilazimisha na sheria za Kiislamu za kusimamisha Swala na kutoa Zaka, basi hao ni ndugu zenu katika Uislamu. Na tunazieleza waziwazi aya na kuzifafanua kwa watu wenye kufaidika nazo. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 9

وَإِن نَّكَثُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُم مِّنۢ بَعۡدِ عَهۡدِهِمۡ وَطَعَنُواْ فِي دِينِكُمۡ فَقَٰتِلُوٓاْ أَئِمَّةَ ٱلۡكُفۡرِ إِنَّهُمۡ لَآ أَيۡمَٰنَ لَهُمۡ لَعَلَّهُمۡ يَنتَهُونَ

Na iwapo washirikina hawa watayavunja makubaliano ambayo mliyowekeana ahadi nao na wakaitukana dini ya Uislamu waziwazi, basi wapigeni vita, kwani wao ni viongozi wa upotevu, hawana ahadi wala dhamana, mpaka wakomeke na ukafiri wao na uadui wao juu ya Uislamu. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 9

أَلَا تُقَٰتِلُونَ قَوۡمٗا نَّكَثُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ وَهَمُّواْ بِإِخۡرَاجِ ٱلرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٍۚ أَتَخۡشَوۡنَهُمۡۚ فَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخۡشَوۡهُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Msiwe kwenye hali ya kutoamua kuhusu kupigana na hawa watu ambao walivunja ahadi zao na wakafanya hima kumtoa Mtume kutoka Maka, na wao ndio walioanza kuwaudhi hapo mwanzo. Je mnawaogopa? Au mnaogopa kupambana nao vitani? Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye haki zaidi ya nyinyi kumuogopa, iwapo kweli nyinyi ni Waumini. info
التفاسير: