ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߊߥߊ߯ߤߟߌߞߊ߲ ߘߟߊߡߌ߬ߘߊ - ߊ߳ߺߓߑߘߎ-ߟߟߊ߯ߤߌ߫ ߡߎ߬ߤߊߡߡߊߘߎ߫ ߣߌ߫ ߣߊ߯ߛ߫ߌߙߎ߫ ߞ߭ߊ߬ߡߌ߯ߛߎ߫ ߓߟߏ߫

ߞߐߜߍ ߝߙߍߕߍ:close

external-link copy
20 : 31

أَلَمۡ تَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَأَسۡبَغَ عَلَيۡكُمۡ نِعَمَهُۥ ظَٰهِرَةٗ وَبَاطِنَةٗۗ وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَلَا هُدٗى وَلَا كِتَٰبٖ مُّنِيرٖ

Kwani hamuoni, enyi watu, kuwa Mwenyezi Mungu amewadhalilishia vilivyoko mbinguni miongoni mwa jua, mwezi, mawingu na vinginevyo, na vilivyoko ardhini miongoni mwa wanyama, miti, maji na vinginevyo visivyodhibitika, na Akaeneza kwenu neema Zake za nje juu ya miili na viungo, na za ndani, kwenye akili na nyoyo, na zile Alizowawekea katika zile msizozijua? Na miongoni mwa watu kuna anayefanya ushindani juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada bila ya hoja wala ubainifu wala kitabu chenye kubainisha kinachofafanua uhakika wa madai yako. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 31

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّبِعُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ بَلۡ نَتَّبِعُ مَا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ٱلشَّيۡطَٰنُ يَدۡعُوهُمۡ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ

Na wakiambiwa hawa wenye kufanya ushindani juu ya kumuwahidisha Mwenyezi Mungu na kumpwekesha kwa ibada, «Fuateni yale Ailiyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Nabii Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,» wanasema, «Bali tutafuata yale tuliyowapata wazazi wetu wako nayo ya ushirikina na kuabudu masanamu.» Je, wanafanya hayo hata kama Shetani anawaita wao, kwa kuwapambia wao matendo yao mabaya na ukanushaji wao Mwenyezi Mungu, kwenye adhabu ya Moto unaowaka? info
التفاسير:

external-link copy
22 : 31

۞ وَمَن يُسۡلِمۡ وَجۡهَهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰۗ وَإِلَى ٱللَّهِ عَٰقِبَةُ ٱلۡأُمُورِ

Na mwenye kumtakasia Mwenyezi Mungu ibada yake na kumkusudia kwake Mola wake Aliyetukuka, na akawa mwema katika maneno yake, mwenye kutengeneza matendo yake, basi huwa ameshikamana na kamba yenye kufikisha kwenye radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo Yake. Na kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake yanakuwa mambo yote, Akamlipa aliye mwema kwa wema wake na aliye mbaya kwa ubaya wake. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 31

وَمَن كَفَرَ فَلَا يَحۡزُنكَ كُفۡرُهُۥٓۚ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ فَنُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Na mwenye kukanusha, usimsikitikie, ewe Mtume, wala usiwe na huzuni, kwa kuwa wewe umetekeleza wajibu wako wa ulinganizi na ufikishaji, kwetu sisi ndio marejeo yao na mwisho wao Siku ya Kiyama, tuwapashe habari ya matendo yao maovu waliyoyafanya duniani, kisha tuwalipe kwa hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yale ambayo nyoyo zao zinayaficha, ya kumkanusha Mwenyezi Mungu na kufadhilisha kumtii Shetani. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 31

نُمَتِّعُهُمۡ قَلِيلٗا ثُمَّ نَضۡطَرُّهُمۡ إِلَىٰ عَذَابٍ غَلِيظٖ

Tutawastarehesha wao kwenye ulimwengu huu wenye kutoweka kwa muda mchache, kisha Siku ya Kiyama tutawawapeleka kwa nguvu na kuwaongoza kwenye adhabu yenye kitisho, nayo ni adhabu ya Jahanamu. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 31

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۚ قُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na lau unawauliza, ewe Mtume, hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, «Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?» Watasema, «Ni Mwenyezi Mungu.» Basi wanaposema hilo, waambie, «Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyeonyesha ushahidi kutoka kwenu nyinyi wenyewe.» Lakini wengi wa hawa washirikina hawaangalii wala hawazingatii ni nani anayestahiki kusifiwa na kushukuriwa , kwa hivyo ndivyo wakamshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 31

لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ

Ni vya Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, vyote vilivyoko mbinguni na ardhini kwa kuvimiliki, kuvifanya vifuate amri, kuvipatisha na kuvipangia mambo yake, hivyo basi hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mkwasi Anayejitosheleza mwenyewe Asiyehitaji viumbe Vyake. Ni Zake Yeye shukrani na sifa njema kwa kila namna. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 31

وَلَوۡ أَنَّمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن شَجَرَةٍ أَقۡلَٰمٞ وَٱلۡبَحۡرُ يَمُدُّهُۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦ سَبۡعَةُ أَبۡحُرٖ مَّا نَفِدَتۡ كَلِمَٰتُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na lau miti ya ardhi yote ingalichongwa ikafanywa kalamu na bahari ikawa ni wino wake, na zikaongezwa juu yake bahari saba, na yakaandikwa, kwa kalamu hizo na wino huo, maneno ya Mwenyezi Mungu yatokanao na ujuzi wake na hukumu Zake na yale ambayo Amewaletea wahyi Malaika Wake na Mitume Wake, zingalivunjika- vunjika kalamu hizo na ungaliisha wino huo, na hayangaliisha maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia ambayo hakuna mwenye kuyazunguka kiujuzi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mshindi Mwenye nguvu katika kuwatesa wanaomshirikisha, ni Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo ya viumbe Vyake. Katika aya hii pana kumthibitishia Mwenyezi Mungu Aliyetukuka sifa ya Maneno kikweli, kama inavyonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 31

مَّا خَلۡقُكُمۡ وَلَا بَعۡثُكُمۡ إِلَّا كَنَفۡسٖ وَٰحِدَةٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٌ

Hakukuwa kuwaumba nyinyi, enyi watu, na kuwafufua Siku ya Kiyama, vile ilivyo nyepesi na rahisi, isipokuwa ni kama kuumba nafsi moja na kuifufua. Hakika Mwenyezi Mungu Anayasikia maneno yenu, Anayaona matendo yenu, na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير: