पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - स्वाहिली अनुवाद : अली मुहसिन बरवानी ।

Al-Buruj

external-link copy
1 : 85

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ

Naapa kwa mbingu yenye Buruji! info

Naapa kwa mbingu yenye Buruj au Manaazil, njia au vituo ambavyo nyota hupitia katika nyendo zake, Buruuj au Manaazil ndio huu mkusanyiko wa nyota unao onekana kwa sura namna mbali mbali mbinguni. Hizo Buruuj zimegawika sehemu kumi na mbili ambazo ardhi inazipitia inapo lizunguka jua.

التفاسير:

external-link copy
2 : 85

وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ

Na kwa siku iliyo ahidiwa! info

Na kwa Siku iliyo ahidiwa kuwa ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo,

التفاسير:

external-link copy
3 : 85

وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ

Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa! info

Na kwa viumbe watao hudhuria Siku hiyo wakaona vitisho na ajabu zitakazo kuwepo,

التفاسير:

external-link copy
4 : 85

قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ

Wameangamizwa watu wa makhandaki. info

Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani watu walio chimba khandaki katika ardhi,

التفاسير:

external-link copy
5 : 85

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ

Yenye moto wenye kuni nyingi! info

Wakawasha moto kuwatumbukiza ndani yake Waumini ili kuwatesa,

التفاسير:

external-link copy
6 : 85

إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ

Walipo kuwa wamekaa hapo! info

Na wao wamekaa ukingoni mwake wakishuhudia mateso yanayo wapata Waumini.

التفاسير:

external-link copy
7 : 85

وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ

Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini. info

Na wao wapo hapo wamehudhuria kwenye mateso wanayo watendea Waumini.

التفاسير:

external-link copy
8 : 85

وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa! info

Na hapana walilo lichukia kwa hao Waumini ila ni kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu ambaye adhabu yake huogopwa, Msifiwa anaye tarajiwa thawabu zake.

التفاسير:

external-link copy
9 : 85

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ

Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu. info

Ambaye, peke yake, ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi anashuhudia yote wayatendayo Waumini na makafiri na atawalipa kwayo.

التفاسير:

external-link copy
10 : 85

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ

Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. info

Hakika walio watia matatani Waumini wanaume na Waumini wanawake kwa maudhi na kuwaadhibu kwa moto, kisha wasitubu na kurejea nyuma watapata Akhera adhabu ya Jahannamu kwa ukafiri wao, na watapata adhabu ya kuunguzwa kwa kule kuwaunguza moto Waumini.

التفاسير:

external-link copy
11 : 85

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ

Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. info

Hakika hao walio kusanya kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu vitendo vyema watapata Mabustani yapitayo mito kati yake. Neema hiyo waliyo lipwa ni kufuzu kukubwa.

التفاسير:

external-link copy
12 : 85

إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ

Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali. info

Hakika mshiko wa Mola wako Mlezi kuwashika majabari umefika ukomo kwa ukali wake

التفاسير:

external-link copy
13 : 85

إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ

Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena, info

Ni Yeye peke yake ndiye Mwenye kuanza kuumba, na kisha ni Yeye anaye rejeza tena,

التفاسير:

external-link copy
14 : 85

وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ

Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi, info

Na Yeye ni Mwingi wa msamaha kwa mwenye kutubu na akarejea, na Mwingi wa mapenzi kwa mwenye kumpenda na akamt'ii.

التفاسير:

external-link copy
15 : 85

ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ

Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu, info

Yeye ndiye Mwenye Kiti cha Enzi na Mwenye kukimiliki, na Mkuu kwa dhati yake na sifa zake.

التفاسير:

external-link copy
16 : 85

فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ

Atendaye ayatakayo. info

Ni Mtendaji kwa alitakalo, na hendi kinyume na uweza wake yeyote anaye taka.

التفاسير:

external-link copy
17 : 85

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ

Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi? info

Je! Imekujia, ewe Muhammad, hadithi ya kile kikundi kilicho a'si katika mataifa yaliyo kwisha pita?

التفاسير:

external-link copy
18 : 85

فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ

Ya Firauni na Thamudi? info

Kaumu ya Firauni na Thamudi na yaliyo washukia katika malipo ya kushikilia kwao upotovu?

التفاسير:

external-link copy
19 : 85

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ

Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha. info

Bali hao makafiri katika kaumu yako ni shadidi zaidi katika kukukadhibisha kuliko hawa walivyo wakadhibisha Mitume wao.

التفاسير:

external-link copy
20 : 85

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ

Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. info

Na Mwenyezi Mungu anawaweza hao, na anawajua vilivyo.

التفاسير:

external-link copy
21 : 85

بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ

Bali hii ni Qur'ani tukufu info

Bali hii ulio waletea ni Qur'ani tukufu inadhihirisha hoja za ukweli wako.

التفاسير:

external-link copy
22 : 85

فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ

Katika Ubao Ulio Hifadhiwa. info

Imo katika Ubao Ulio Hifadhiwa, hapana uwezo unao weza kuipotoa au kuigeuza

التفاسير: