पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - स्वाहिली अनुवाद : अली मुहसिन बरवानी ।

Al-Aadiyat

external-link copy
1 : 100

وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحٗا

Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, info

Ninaapa kwa farasi wa Jihadi wendao mbio, na huku pumzi zao zinasikilizana kwa sauti inayo itwa "Dh'abh'an".

التفاسير:

external-link copy
2 : 100

فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحٗا

Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, info

Na kwa farasi hao ambao hutoa cheche za moto zinapo gonga kwato zao kwenye ardhi wanapo kwenda.

التفاسير:

external-link copy
3 : 100

فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحٗا

Wakishambulia wakati wa asubuhi, info

Na kwa farasi hao wanao washambulia maadui asubuhi kabla jua halijachomoza;

التفاسير:

external-link copy
4 : 100

فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعٗا

Huku wakitimua vumbi, info

Wakatimua mavumbia mengi, farasi hao, kati ya makundi ya maadui!

التفاسير:

external-link copy
5 : 100

فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا

Na wakijitoma kati ya kundi, info

Ikawa vumbi limewagubika maadui hata wakaingiwa kiwewe na kufazaika.

التفاسير:

external-link copy
6 : 100

إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٞ

Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! info

Hakika mwanaadamu ni mwingi wa kuzikufuru neema za Mola wake Mlezi ambazo hazikadiriki.

التفاسير:

external-link copy
7 : 100

وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٞ

Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! info

Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka atakuwa mwingi wa kuja jishuhudia huko Akhera kwa kuungama madhambi yake.

التفاسير:

external-link copy
8 : 100

وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلۡخَيۡرِ لَشَدِيدٌ

Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! info

Na hakika yeye kwa uchoyo na kuyapenda mali alio nayo, ni bakhili, hatoi kama inavyo mwajibikia katika mali yake.

التفاسير:

external-link copy
9 : 100

۞ أَفَلَا يَعۡلَمُ إِذَا بُعۡثِرَ مَا فِي ٱلۡقُبُورِ

Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? info

Kwani hajui mwisho wa hali yake, hata hajui wakitolewa maiti waliomo makaburini,

التفاسير:

external-link copy
10 : 100

وَحُصِّلَ مَا فِي ٱلصُّدُورِ

Na yakakusanywa yaliomo vifuani? info

Na vikakusanywa viliomo vifuani navyo vimekwisha sajiliwa katika madaftari yao, yakiwa mema au mabaya waliyo yatenda?

التفاسير:

external-link copy
11 : 100

إِنَّ رَبَّهُم بِهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّخَبِيرُۢ

Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! info

Kwamba hakika Mlezi wao na Muumba wao bila ya shaka anajua vyema vitendo vyao na malipo yao Siku ya Kufufuliwa na Kulipwa.

التفاسير: