पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - सवाहिली अनुवाद : अब्दुल्लाह मुहम्मद र नासिर खमीस

At-Tariq

external-link copy
1 : 86

وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu na nyota yenye kuchomoza usiku. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 86

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ

Na ni lipi lilokujulisha ni ukubwa gani wa nyota hiyo? info
التفاسير:

external-link copy
3 : 86

ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ

Hiyo ni nyota ing’arao na kuzagaa. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 86

إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ

Hakuna nafsi yoyote isipokuwa amewakilishwa kwayo Malaika mwenye kuchunguza na kusjili amali zake ili ihesabiwe Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 86

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ

Basi aangalie binadamu mwenye kukanusha kufufuliwa ameumbwa kwa kitu gani? Ili ajue kuwa kurudisha umbo lake mara ya pili si vigumu kama kuumbwa mara ya kwanza. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 86

خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ

Aliumbwa kwa manii yenye kupenyeza ndani ya uzao kwa haraka. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 86

يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ

Yatokayo kwenye mgongo wa mwnamume na kifua cha mwanamke. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 86

إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ

Hakika yule Aliyemuumba binadamu kwa maji haya ni muweza wa kumrudisha kwenye uhai baada ya kufa. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 86

يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ

Siku zitakapofunuliwa wazi siri ziliofichwa na nafsi na kupambanuliwa njema na mbovu. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 86

فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ

Binadamu hatakuwa na nguvu ya kuitetea nafsi yake wala hatakuwa na mtetezi wa kumwepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 86

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ

Na Anaapa kwa mbingu yenye mvua ya kukaririka. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 86

وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ

Na ardhi yenye pasuko za kufanya mimea ichipuke. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 86

إِنَّهُۥ لَقَوۡلٞ فَصۡلٞ

Hakika Qur’ani ni neno lenye kupambanua baina ya haki na batili. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 86

وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ

Na si upuuzi. Haifai kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Akifanya hivyo atakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 86

إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدٗا

Hakika wenye kumkanusha Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Qur’ani wanafanya vitimbi na mipango ili kuipinga haki na kuitilia nguvu batili. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 86

وَأَكِيدُ كَيۡدٗا

Na Mimi nafanya vitimbi kuidhihirisha haki ingawa makafiri wanatukia.Usiwe na haraka nao, ewe Mtume, kutaka wateremshiwe adhabu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 86

فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا

Wape muhula uwangojee muda mchache wala usiwafanyie haraka, utaona adhabu itakayowafikia, mateso na maangamivu. info
التفاسير: