पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - सवाहिली अनुवाद : अब्दुल्लाह मुहम्मद र नासिर खमीस

external-link copy
15 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ زَحۡفٗا فَلَا تُوَلُّوهُمُ ٱلۡأَدۡبَارَ

Enyi wale ambao walimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafuata sheria Yake kivitendo, mpambanapo na waliokanusha katika vita wakawa wanasongea karibu yenu msiwape migongo yenu na mkakubali kushindwa na wao, lakini kuweni imara na wao, kwani Mwenyezi Mungu yuko pamoja na nyinyi na ni Mwenye kuwapa ushindi juu yao. info
التفاسير: