पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - सवाहिली अनुवाद : अब्दुल्लाह मुहम्मद र नासिर खमीस

رقم الصفحة:close

external-link copy
53 : 8

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ لَمۡ يَكُ مُغَيِّرٗا نِّعۡمَةً أَنۡعَمَهَا عَلَىٰ قَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِهِمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Malipo hayo maovu ni kwamba Mwenyezi Mungu pindi Anapowaneemesha watu neema yoyote, hawaondolei mpaka wabadilishe hali yao njema iwe mbovu, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzijua hali zao, kwa hivyo huwapitishia yale yaliyolingana na ujuzi Wake na matakwa Yake. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 8

كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ فَأَهۡلَكۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَۚ وَكُلّٞ كَانُواْ ظَٰلِمِينَ

Hali ya Makafiri hawa ni kama hali ya Makafiri wa jamaa za Fir'awn ambao walimkanusha Mūsā, na ni kama hali ya wale waliowakanusha Mitume wao miongoni mwa watu waliopita. Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza kwa sababu ya madhambi yao na Akawazamisha jamaa za Fir'awn baharini. Na kila umma kati yao walikuwa wanatenda mambo ambayo haikufaa wao kuyatenda, ya kukanusha kwao Mitume wa Mwenyezi Mungu na kupinga kwao aya za Mwenyezi Mungu na kushirikisha kwao, katika ibada, asiyekuwa Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 8

إِنَّ شَرَّ ٱلدَّوَآبِّ عِندَ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hakika wabaya mno wa wale wanaotembea juu ya ardhi mbele ya Mwenyezi Mungu ni Makafiri wanaoendeleza ukafiri; wao hawawaamini Mitume wa Mwenyezi Mungu, hawaukubali upweke Wake wala hawazifuati sheria Zake. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 8

ٱلَّذِينَ عَٰهَدتَّ مِنۡهُمۡ ثُمَّ يَنقُضُونَ عَهۡدَهُمۡ فِي كُلِّ مَرَّةٖ وَهُمۡ لَا يَتَّقُونَ

Miongoni mwa wabaya hao ni Mayahudi ambao waliingia pamoja na wewe katika mapatano kwamba hawatakupiga vita wala hawatamsaidia yoyote dhidi yako, kisha wanazivunja ahadi zao mara kwa mara hali ya kuwa wao hawamuogopi Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 8

فَإِمَّا تَثۡقَفَنَّهُمۡ فِي ٱلۡحَرۡبِ فَشَرِّدۡ بِهِم مَّنۡ خَلۡفَهُمۡ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ

Pindi utakapopambana na hawa, wanaovunja ahadi na mapatano, katika vita, wape adhabu ambayo itatia kicho kwenye nyoyo za wegine na itaitawanya mikusanyiko yao, huenda wao wakazingatia wasiwe na ujasiri wa kufanya kama yale waliyoyafanya waliotangulia. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 8

وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوۡمٍ خِيَانَةٗ فَٱنۢبِذۡ إِلَيۡهِمۡ عَلَىٰ سَوَآءٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡخَآئِنِينَ

Na ukiogopa, ewe Mtume, hiana ambayo ishara zake zimejitokeza, kutoka kwa kundi lolote, basi watupilie mbali ahadi yao, ili zote pande mbili ziwe zimelingana kwa kujua kwamba hapana tena mapatano baada ya leo. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kuenda kinyume na ahadi zao, wavunjaji ahadi na mapatano. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 8

وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ سَبَقُوٓاْۚ إِنَّهُمۡ لَا يُعۡجِزُونَ

Na wasidhanie wale ambao walizikanusha aya za Mwenyezi Mungu kwamba wao washapita na washaokoka na kwamba Mwenyezi Mungu Hawawezi; hakika wao hawatakwepa adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 8

وَأَعِدُّواْ لَهُم مَّا ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن قُوَّةٖ وَمِن رِّبَاطِ ٱلۡخَيۡلِ تُرۡهِبُونَ بِهِۦ عَدُوَّ ٱللَّهِ وَعَدُوَّكُمۡ وَءَاخَرِينَ مِن دُونِهِمۡ لَا تَعۡلَمُونَهُمُ ٱللَّهُ يَعۡلَمُهُمۡۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يُوَفَّ إِلَيۡكُمۡ وَأَنتُمۡ لَا تُظۡلَمُونَ

Na Tayarisheni, enyi makundi ya Waislamu,ili kukabiliana na maadui wenu, chochote mkiwezacho cha wingi wa watu na zana, ili muingize, kwa hio, kicho katika nyoyo za maadui wa Mwenyezi mungu na maadui wenu wanaowavizia; na muwatishe wengine ambao uadui wao bado haujajitokeza kwenu hivi sasa, lakini Mwenyezi Mungu Anawajua na Anayajua yale ambayo wanayadhamiria. Na mali yoyote na vinginevyo mnavyovitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, vingi au vichache, Mwenyezi Mungu Atawapa badala yake duniani na Atawaekea thawabu zake mpaka Siku ya Kiyama; na nyinyi hamtapunguziwa malipo ya hayo chochote. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 8

۞ وَإِن جَنَحُواْ لِلسَّلۡمِ فَٱجۡنَحۡ لَهَا وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na wakielekea kuacha vita na wakapendelea kuishi kwa amani na nyinyi, basi nawe elekea huko, ewe Nabii, na uyategemeze mambo yako kwa Mwenyezi Mungu na uwe na imani na Yeye. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kuyasikia maneno yao, Mwenye kuzijua nia zao. info
التفاسير: