पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - सवाहिली अनुवाद : अब्दुल्लाह मुहम्मद र नासिर खमीस

رقم الصفحة:close

external-link copy
12 : 57

يَوۡمَ تَرَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ يَسۡعَىٰ نُورُهُم بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَبِأَيۡمَٰنِهِمۖ بُشۡرَىٰكُمُ ٱلۡيَوۡمَ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Siku utakapowaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike ikitembea nuru yao juu ya njia ya Ṣirāṭ mbele yao na upande wao wa kulia kwa kadiri ya matendo yao mema na waambiwe, «Bishara yenu leo ni kuingia kwenye mabustani ya Peponi yaliyo makunjufu ambayo chini ya miti yake inapita mito, hamtatolewa humo milele.» Malipo hayo ndiyo kufuzu kwenu kukubwa huko Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 57

يَوۡمَ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱنظُرُونَا نَقۡتَبِسۡ مِن نُّورِكُمۡ قِيلَ ٱرۡجِعُواْ وَرَآءَكُمۡ فَٱلۡتَمِسُواْ نُورٗاۖ فَضُرِبَ بَيۡنَهُم بِسُورٖ لَّهُۥ بَابُۢ بَاطِنُهُۥ فِيهِ ٱلرَّحۡمَةُ وَظَٰهِرُهُۥ مِن قِبَلِهِ ٱلۡعَذَابُ

Siku watakaposema wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike wakiwaambia Waumini, «Tungojeeni tupate mwangaza wa nuru yenu!» Hapo Malaika wawaambie, «Rudini nyuma yenu mtafute nuru (kwa njia ya kuwafanyia shere). Hapo watenganishwe baina yao kwa kuwekwa kizuizi cha ukuta wenye mlango ambao ndani yake , upande wa Waumini, mna rehema, na nje yake, upande wa wanafiki kuna adhabu. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 57

يُنَادُونَهُمۡ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ وَلَٰكِنَّكُمۡ فَتَنتُمۡ أَنفُسَكُمۡ وَتَرَبَّصۡتُمۡ وَٱرۡتَبۡتُمۡ وَغَرَّتۡكُمُ ٱلۡأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَآءَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَغَرَّكُم بِٱللَّهِ ٱلۡغَرُورُ

Hapo wale wanafiki wawaite Waumini kwa kusema, «Kwani hatukuwa na nyinyi duniani tukitekeleza ibada za Dini kama nyinyi?» Na Waumini wawaambie, «Ndio, mlikuwa na sisi kidhahiri, lakini nyinyi mlijiangamiza wenyewe kwa unafiki na kufanya maasia, na mkingojea kwa hamu Nabii afe na Waumini wapatikane na mikasa, mkakufanyia shaka kule kufufuliwa baada ya kufa, na yakawadanganya nyinyi matumaini yenu ya urongo na mkasalia katika hali hiyo mpaka mauti yakawajia. Na Shetani aliwadanganya nyinyi kuhusu Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 57

فَٱلۡيَوۡمَ لَا يُؤۡخَذُ مِنكُمۡ فِدۡيَةٞ وَلَا مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ مَأۡوَىٰكُمُ ٱلنَّارُۖ هِيَ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Leo haitakubaliwa badala kutoka kwa yoyote miongoni mwenu, enyi wanafiki, ili ajifidie kwayo na adhabu ya Mwenyezi Mungu wala kutoka kwa wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. mwisho wenu nyote ni Moto, huo ni makao mnayostahili zaidi kuliko makao yoyote, na mwisho mbaya kabisa ni huo. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 57

۞ أَلَمۡ يَأۡنِ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن تَخۡشَعَ قُلُوبُهُمۡ لِذِكۡرِ ٱللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ ٱلۡحَقِّ وَلَا يَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلُ فَطَالَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَمَدُ فَقَسَتۡ قُلُوبُهُمۡۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ

Je haujafika wakati kwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakafuata uongofu Wake kulainika nyoyo zao anapotajwa Mwenyezi Mungu na kuisikia Qur’ani, na wasiwe ni wenye ugumu wa nyoyo kama walivyokuwa wale waliopewa Vitabu kabla yao, kati ya Mayahudi na Wanaswara, ambao walipitiwa na muda mrefu wakayageuza maneno ya Mwenyezi Mungu na nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi miongoni mwao wakatoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu? Katika aya hii pana kuhimiza ulainifu na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, wakati wa kuyasikia yale Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ya Kitabu na Hekima, na kujihadhari na kujifananisha na Mayahudi na Wanaswara katika ususuwavu wa nyoyo zao na kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 57

ٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يُحۡيِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَاۚ قَدۡ بَيَّنَّا لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Jueni kwamba Mwenyezi mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Anaihuisha ardhi kwa mvua baada ya kufa kwake ikatoa mimea. Basi vilevile Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuhuisha wafu Siku ya Kiyama, na Ndiye Muweza wa kuzilainisha nyoyo baada ya kususuwaa kwake. Kwa hakika tumewafunulia wazi dalili za uweza wetu, huenda nyinyi mkazielewa na kwa hivyo mkawaidhika. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 57

إِنَّ ٱلۡمُصَّدِّقِينَ وَٱلۡمُصَّدِّقَٰتِ وَأَقۡرَضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا يُضَٰعَفُ لَهُمۡ وَلَهُمۡ أَجۡرٞ كَرِيمٞ

Hakika ya wale wanaume na wanawake wanaotoa sadaka kutokana na mali yao na wakatumia katika njia ya Mwenyezi Mungu matumizi zikiwa radhi nyoyo zao, kwa kutafuata radhi za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, wataongezewa malipo mema ya hayo, na juu ya hayo watapata malipo mengi, nayo ni Pepo. info
التفاسير: