पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - सवाहिली अनुवाद : अब्दुल्लाह मुहम्मद र नासिर खमीस

Qaf

external-link copy
1 : 50

قٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡمَجِيدِ

«Qāf» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzoni mwa sura ya Al-Baqarah. Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Qur’ani tukufu, yenye ubora na heshima. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 50

بَلۡ عَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٞ مِّنۡهُمۡ فَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا شَيۡءٌ عَجِيبٌ

Bali wale wenye kumkanusha Mtume waliona ajabu kuwa walijiwa na muonyaji miongoni mwao anayewaonya mateso ya Mwenyezi Mungu, basi wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walisema, «Hili ni jambo geni la kuonewa ajabu. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 50

أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗاۖ ذَٰلِكَ رَجۡعُۢ بَعِيدٞ

«Je, tunapokufa na tukawa mchanga, itawezekana vipi kurejea baada ya hapo tukawa kama tulivyokuwa? Hayo ni marajeo ambayo kutukia kwake kuko mbali.» info
التفاسير:

external-link copy
4 : 50

قَدۡ عَلِمۡنَا مَا تَنقُصُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۡهُمۡۖ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظُۢ

Hakika tunakijua kile ambacho ardhi kinakipunguza na kukimaliza katika miili yao, na tuna Kitabu kilichohifadhiwa kutokana na mageuzo na mabadiliko, kilichosajiliwa kila kitu kitakachowapitia katika maisha yao na baada ya kufa kwao. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 50

بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَهُمۡ فِيٓ أَمۡرٖ مَّرِيجٍ

Bali hawa washirikina waliikanusha Qur’ani ilipowajia. Wao wako kwenye hali ya babaiko na kuchanganyikiwa, hawasimami imara kwenye jambo lolote, na hawana kituo cha kutulia. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 50

أَفَلَمۡ يَنظُرُوٓاْ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوۡقَهُمۡ كَيۡفَ بَنَيۡنَٰهَا وَزَيَّنَّٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٖ

Kwani walighafilika walipokanusha Ufufuzi, wasianagalie mbingu juu yao: vipi tulizijenga zikiwa zimelingana sawa pande zote, limeimarika jengo lake, na tukazipamba kwa nyota, na hazina pasuko na nyufa, zimesalimika na hitilafu na kasoro? info
التفاسير:

external-link copy
7 : 50

وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجِۭ بَهِيجٖ

Na ardhi tumeipanua na kuitandika, na tukaweka humo majabali yaliyojikita, ili ardhi isiende mrama na watu wake, na tukaotesha humo kila aina ya mimea yenye mandhari ya kupendeza na yenye kunufaisha, inayomfurahisha mwenye kuiangalia. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 50

تَبۡصِرَةٗ وَذِكۡرَىٰ لِكُلِّ عَبۡدٖ مُّنِيبٖ

Mwenyezi Mungu Ameumba mbingu, ardhi na vilivyomo baina ya hivyo viwili miongoni mwa alama kubwa, ili viwe ni mazingatio ya kumfanya mtu aone na atoke kwenye giza la ujinga, na ni ukumbusho kwa kila mja mnyenyekevu, mwenye kucha na kuogopa, mwenye kurejea sana kwa Mwenyezi Mungu Aliyeshinda na kutukuka. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 50

وَنَزَّلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ مُّبَٰرَكٗا فَأَنۢبَتۡنَا بِهِۦ جَنَّٰتٖ وَحَبَّ ٱلۡحَصِيدِ

Na tumeteremsha kutoka juu mvua yenye manufaa mengi, tukaotesha kwayo mabustani yenye miti mingi na nafaka za mimea ya nafaka zinazovunwa. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 50

وَٱلنَّخۡلَ بَاسِقَٰتٖ لَّهَا طَلۡعٞ نَّضِيدٞ

Na tukaotesha mitende mirefu yenye makarara yaliyojaza na kupandana. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 50

رِّزۡقٗا لِّلۡعِبَادِۖ وَأَحۡيَيۡنَا بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗاۚ كَذَٰلِكَ ٱلۡخُرُوجُ

Tumeviotesha hivyo viwe ni riziki za waja za wao kuzila kulingana na mahitaji yao, na tukahuisha, kwa maji haya tuliyoyateremsha, ardhi iliyokuwa kavu na kame, haina nafaka wala mimea mingine. Na kama tunavyohuisha, kwa maji hayo, ardhi iliyokufa, tutawatoa nyinyi Siku ya Kiyama mkiwa hai baada ya kufa. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 50

كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَأَصۡحَٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ

Walikanusha, kabla ya hawa washirikina miongoni mwa Makureshi, watu wa Nūḥ, watu wa Kisima na Thamūd. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 50

وَعَادٞ وَفِرۡعَوۡنُ وَإِخۡوَٰنُ لُوطٖ

Na 'Ād na Fir'awn na watu wa Lūṭ. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 50

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ وَقَوۡمُ تُبَّعٖۚ كُلّٞ كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ

Na watu waliokuwa kwenye tuka la miti nao ni watu wa Shu'ayb, na watu wa Tubba' wa Himyar. Watu wote hao waliwakanusha Mitume wao, ikapasa juu yao adhabu ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaonya nayo kwa ukafiri wao. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 50

أَفَعَيِينَا بِٱلۡخَلۡقِ ٱلۡأَوَّلِۚ بَلۡ هُمۡ فِي لَبۡسٖ مِّنۡ خَلۡقٖ جَدِيدٖ

Kwani tulishindwa kuanzisha uumbaji wa kwanza tuliyouanzisha na hakukuwa na kitu chochote, mpaka tushindwe kuwarudisha wao wakiwa viumbe wapya baada ya kutoweka kwao? Hilo halitushindi. Bali sisi ni waweza wa hilo, lakini wao wako kwenye mshangao na shaka juu ya jambo la kufufuliwa na kukusanywa. info
التفاسير: