पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - सवाहिली अनुवाद : अब्दुल्लाह मुहम्मद र नासिर खमीस

Yasin

external-link copy
1 : 36

يسٓ

«Yā Sīn» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 36

وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡحَكِيمِ

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Qur’ani yenye hekima, kwa hukumu zilizomo, hekima na hoja, info
التفاسير:

external-link copy
3 : 36

إِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

kwamba wewe, ewe Mtume, ni miongoni mwa waliotumilizwa na wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake, info
التفاسير:

external-link copy
4 : 36

عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

juu ya njia iliyonyoka na kulingana sawa, nayo ni Uislamu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 36

تَنزِيلَ ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

Ameiteremsha Mwenyezi Mungu hii Qur’ani ikiwa ni teremsho kutoka kwa Aliye Mshindi, katika kuwaadhibu watu wa ukafiri na maasia, Mwenye kuwarehemu waja Wake waliotubia na wakatenda mema. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 36

لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمۡ فَهُمۡ غَٰفِلُونَ

Tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, ili uwaonye nayo watu ambao baba zao kabla yako wewe hawakuonya, nao ni Warabu. Watu hawa wameghafilika na wamepitikiwa na Imani na msimamo imara wa kufanya matendo mema. Na kila watu ambao uonyaji kwao umekatika, wanaingia kwenye mghafala na kupitikiwa. Katika haya kuna dalili ya ulazima juu ya wanavyuoni, wanaomjua Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kulingania na kukumbusha, ili wawaamshe Waislamu kutoka kwenye mghafala wao. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 36

لَقَدۡ حَقَّ ٱلۡقَوۡلُ عَلَىٰٓ أَكۡثَرِهِمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hakika imeshapasa adhabu juu ya wengi wa hawa makafiri, baada ya kuonyeshwa haki wakaikataa, kwa kuwa hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Mtume Wake wala hawafuati Sheria Zake kivitendo. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 36

إِنَّا جَعَلۡنَا فِيٓ أَعۡنَٰقِهِمۡ أَغۡلَٰلٗا فَهِيَ إِلَى ٱلۡأَذۡقَانِ فَهُم مُّقۡمَحُونَ

Hakika sisi tumewafanya hawa makafiri, ambao walionyeshwa haki wakaikataa na wakawa wakakamavu kushikilia ukafiri na kuacha kuamini, ni kama wale waliofungwa pingu shingoni mwao, ikakusanywa pamoja mikono yao pamoja na shingo zao chini ya videvu vyao, wakalazimika kuinua juu vichwa vyao. Basi wao wamefungwa na kuepushwa na kila kheri, hawaioni haki wala hawaongoki kuifuata. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 36

وَجَعَلۡنَا مِنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ سَدّٗا وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ سَدّٗا فَأَغۡشَيۡنَٰهُمۡ فَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ

Na tumeweka mbele ya makafiri kizuizi na nyuma yao kizuizi. Basi yeye ni kama wale waliyofungiwa njia mbele yao na nyuma yao, hapo tukayapofusha macho yao kwa sababu ya ukanushaji wao na kiburi chao, hivyo basi wakawa hawaoni usawa wala hawaongoki. Na kila mwenye kuukabili ulinganizi wa Uislamu kwa kuupa mgongo na kuufanyia ushindani, basi yeye ni mstahili wa kupata mateso haya. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 36

وَسَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ ءَأَنذَرۡتَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تُنذِرۡهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Kunalingana sawa, mbele ya makafiri hawa washindani, kuwa utawaonya, ewe Mtume, au hutawaonya, kwani wao hawaamini wala hawafanyi matendo mema. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 36

إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكۡرَ وَخَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِۖ فَبَشِّرۡهُ بِمَغۡفِرَةٖ وَأَجۡرٖ كَرِيمٍ

Hakika ni kwamba uonyaji wako unamfaa mwenye kuiamini Qur’ani, akafuata hukumu za Mwenyezi Mungu zilizo ndani yake na akamuogopa Mwingi wa rehema akiwa mahali ambapo hakuna amuonaye isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi huyo mpe bishara njema ya kuwa atapata msamaha wa dhambi zake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na atapata malipo mema kutoka Kwake huko Akhera kwa matendo yake mema, nayo ni Pepo. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 36

إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَنَكۡتُبُ مَا قَدَّمُواْ وَءَاثَٰرَهُمۡۚ وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ فِيٓ إِمَامٖ مُّبِينٖ

Hakika sisi ndio tunaohuisha wafu wote kwa kuwafufua Siku ya Kiyama, na tunaandika waliyoyafanya ya kheri na shari, na zile athari zao njema ambazo wao walikuwa ndio sababu ya kufanyika katika maisha yao na baada ya kufa kwao, ziwe njema kama vile mtoto mwema, elimu yenye manufaa na sadaka yenye kuendelea, na ziwe mbaya kama vile ushirikina na uasi. Na tumedhibiti kwa hesabu kila kitu katika Kitabu chenye ufafanuzi, ambacho ni Asili ya Kitabu, na humo ndio marejeo ya yote hayo, nacho ni Ubao Uliohifadhiwa. Basi ni juu ya mwenye akili airudie nafsi yake, ili awe ni kiigizo katika wema ndani ya maisha yake na baada ya kufa kwake. info
التفاسير: