വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് തർജമ സെൻ്റർ

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
179 : 7

وَلَقَدۡ ذَرَأۡنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِۖ لَهُمۡ قُلُوبٞ لَّا يَفۡقَهُونَ بِهَا وَلَهُمۡ أَعۡيُنٞ لَّا يُبۡصِرُونَ بِهَا وَلَهُمۡ ءَاذَانٞ لَّا يَسۡمَعُونَ بِهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ

Na hakika tumeiumbia Jahannamu wengi katika majini na watu. Wana nyoyo wasizofahamu kwazo. Na wana macho wasiyoona kwayo. Na wana masikio wasiyosikia kwayo. Hao ni kama wanyama wa mifugo, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. info
التفاسير:

external-link copy
180 : 7

وَلِلَّهِ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ فَٱدۡعُوهُ بِهَاۖ وَذَرُواْ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ أَسۡمَٰٓئِهِۦۚ سَيُجۡزَوۡنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopindukia mipaka katika majina yake. Watakuja lipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
181 : 7

وَمِمَّنۡ خَلَقۡنَآ أُمَّةٞ يَهۡدُونَ بِٱلۡحَقِّ وَبِهِۦ يَعۡدِلُونَ

Na katika wale tuliowaumba wako umma wanaoongoza kwa haki, na kwayo wanafanya uadilifu. info
التفاسير:

external-link copy
182 : 7

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ

Na wale waliokadhibisha Ishara zetu, tutawapeleka katika maangamio pole pole kutokea pale wasipojua. info
التفاسير:

external-link copy
183 : 7

وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ

Nami nitawapa muda. Hakika njama yangu ni madhubuti. info
التفاسير:

external-link copy
184 : 7

أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٌ

Je, hawafikirii? Huyu mwenzao hana wazimu. Yeye siyo isipokuwa ni mwonyaji aliye dhahiri. info
التفاسير:

external-link copy
185 : 7

أَوَلَمۡ يَنظُرُواْ فِي مَلَكُوتِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ وَأَنۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَدِ ٱقۡتَرَبَ أَجَلُهُمۡۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ

Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi, na vile vyote alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika vitu, na kwamba huenda muda wao umekwisha karibia? Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? info
التفاسير:

external-link copy
186 : 7

مَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَا هَادِيَ لَهُۥۚ وَيَذَرُهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Yule Mwenyezi Mungu alimpoteza, basi hana wa kumwongoa. Atawaacha hao katika upotovu wao wakitangatanga. info
التفاسير:

external-link copy
187 : 7

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّيۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقۡتِهَآ إِلَّا هُوَۚ ثَقُلَتۡ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا تَأۡتِيكُمۡ إِلَّا بَغۡتَةٗۗ يَسۡـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنۡهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanakuuliza kuhusu hiyo Saa (ya Qiyama) kusimama kwake ni lini? Sema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitawajia isipokuwa kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Elimu yake iko tu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wa watu hawajui. info
التفاسير: