വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി പരിഭാഷ - അലി മുഹ്സിൻ അൽബർവാനി

external-link copy
77 : 5

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ غَيۡرَ ٱلۡحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوٓاْ أَهۡوَآءَ قَوۡمٖ قَدۡ ضَلُّواْ مِن قَبۡلُ وَأَضَلُّواْ كَثِيرٗا وَضَلُّواْ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki. Wala msifuate matamanio ya watu walio kwisha potea tangu zamani, na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa. info

Ewe Mtume! Waambie Watu wa Kitabu, yaani Mayahudi na Wakristo: Mwenyezi Mungu anakukatazeni msivuke mipaka katika itikadi zenu hata mkaingia katika upotovu, mkawafanya baadhi ya viumbe vyake kuwa ni miungu; au mkakanusha ujumbe wa baadhi ya Mitume. Na anakukatazeni kufuata matamanio ya watu walio kutangulieni, walio acha njia ya uwongofu, na wakawazuia watu wengi kuifuata njia hiyo, na wakaendelea katika kuiepuka Njia ya Haki.

التفاسير: