വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി പരിഭാഷ - അലി മുഹ്സിൻ അൽബർവാനി

external-link copy
14 : 4

وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُۥ يُدۡخِلۡهُ نَارًا خَٰلِدٗا فِيهَا وَلَهُۥ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha. info

Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akaikiuka mipaka aliyo iweka Mwenyezi Mungu, na huku akihalalisha kukiuka huko basi mtu huyo atalipwa Moto, na humo atakaa milele, akiadhibiwa mwili wake juu ya kuadhibiwa roho yake.

التفاسير: