വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

Al-Buruj

external-link copy
1 : 85

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mbingu zenye njia za kupitia jua na mwezi. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 85

وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ

Na kwa Siku ya Kiyama ambayo Amewaahidi viumbe kuwa Atawakusanya. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 85

وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ

Na kwa shahidi, mwenye kutoa ushahidi, na mwenye kutolewa ushahidi juu yake. Mwenyezi Mungu Huapa kwa Anachokitaka. Lakini kiumbe hafai kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 85

قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ

Wamelaaniwa waliofukua chini ya ardhi shimo kubwa ili kuwatesa Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 85

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ

Wakawasha moto mkubwa wenye kuni nyingi. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 85

إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ

Wakawa wamekaa kwenye kingo za shimo hilo. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 85

وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ

Wakishuhudia vitendo vya mateso na adhabu wanavyowafanyia Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 85

وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Na hawakuwatesa mateso hayo isipokuwa wenye kuteswa walikuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu Mshindi Asiyeshindwa, Mhimidiwa wa maneno Yake vitendo Vyake na sifa Zake. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 85

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ

Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi Ambaye, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Anashuhudia kila kitu, hakuna kinachofichika kwake. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 85

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ

Hakika, wale waliowachoma kwa moto Waumini, wa kike na wa kiume, ili kuwazuia watu na dini ya Mwenyezi Mungu, kisha wasitubie, watapata, Siku ya Akhera, adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu kali yenye kuchoma. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 85

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ

Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya amali njema, watapata Pepo ambayo chini ya majumba yake ya kifahari yapita mito. Huko ni kufaulu kukubwa. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 85

إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ

Hakika malipizo ya Mola wako kwa maadui Zake na mateso Yake juu yao ni mazito. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 85

إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ

Ndiye Yeye Mwenye kuanzisha kuumba na kisha kurudisha. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 85

وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ

Ndiye Yeye Mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia, Mwingi wa mapenzi kwa wanaoikurubisha kwake. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 85

ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ

Mwenye Arshi tukufu. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 85

فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ

Mfanya Alitakalo: hakuna kitu Anachotaka kiwe kisiwe. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 85

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ

Je, ewe Mtume, imekufikia habari ya makundi yaliyokufuru na kukanusha Mitume walioletwa, ya info
التفاسير:

external-link copy
18 : 85

فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ

Firauni na Thamūd, misiba na adhabu iliyowashukia? Hawakuzingatia kwa habari hiyo. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 85

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ

Bali waliokufuru waendelea kukanusha kwao, kama walivyokuwa waliokuja kabla yao. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 85

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ

Na Mwenyezi Mungu Amewazunguka kwa Ujuzi na Uweza Wake, hakuna chenye kufichika Kwake kuhusu wao na vitendo vyao. Hii Qu’ani siyo kama wanavyodai wenye kukanusha katika washirikina kuwa ni mashairi na uchawi ndipo wakaikanusha. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 85

بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ

Bali hii ni Qur’ani kubwa iliyo tukufu, info
التفاسير:

external-link copy
22 : 85

فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ

iliyomo kwenye Ubao Uliohifadhiwa, haufikiwi na kubadilishwa wala kupotoshwa. info
التفاسير: