വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

Al-Anfal

external-link copy
1 : 8

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَنفَالِۖ قُلِ ٱلۡأَنفَالُ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَصۡلِحُواْ ذَاتَ بَيۡنِكُمۡۖ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Masahaba Zako wanakuuliza, ewe Nabii, kuhusu ngawira siku ya Badr: utawagawia vipi? Waambie, «Jambo lake limeachiwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake» Mtume ndiye mwenye kusimamia ugawaji wake kwa amri ya Mola wake. Basi jikingeni na mateso ya Mwenyezi Mungu wala msithubutu kumuasi, na muache kubishana na kuteta kwa sababu ya mali, na mzitengeneze hali zenu, na mjilazimishe utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake iwapo nyinyi ni Waumini, kwani Imani inapelekea kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 8

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَإِذَا تُلِيَتۡ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Hakika wenye kumuamini Mwenyezi Mungu kikweli ni wale ambao akitajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao zinaingiwa na kicho, wasomewapo aya za Mwenyezi Mungu zinawazidishia Imani pamoja na Imani waliyo nayo kwa kuyazingatia maana yake na kwa Mola wao wanategemea: hawamtaraji isipokuwa Yeye na hawamuogopi isipokuwa Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 8

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ

Wale ambao wanaendelea kutekeleza Swala zilizofaradhiwa kwa nyakati zake, na katika kile tulichowaruzuku wanatoa kwenye yale tuliyowaamrisha. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 8

أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ حَقّٗاۚ لَّهُمۡ دَرَجَٰتٌ عِندَ رَبِّهِمۡ وَمَغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ

Hawa wanaofanya matendo haya ndio wenye kuyaamini kikweli, nje na dani, yale Aliyowateremshia Mwenyezi Mungu, watakuwa na daraja za juu mbele ya Mwenyezi Mungu, msamaha wa dhambi zao na riziki nzuri ambayo ni Pepo. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 8

كَمَآ أَخۡرَجَكَ رَبُّكَ مِنۢ بَيۡتِكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لَكَٰرِهُونَ

Na kama mlivyotafautiana juu ya ugawaji wa ngawira, na Mwenyezi Mungu Akauondoa kwenu na Akauweka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, rehema na amani zimshukiye, hivyo ndivyo Mola wako Alivyokuamrisha utoke Madina uende kupambana na msafara wa Makureshi kwa wahyi aliyokujia nao Jibrili, pamoja na kuwa kundi miongoni mwa Waumini walichukia kutoka. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 8

يُجَٰدِلُونَكَ فِي ٱلۡحَقِّ بَعۡدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى ٱلۡمَوۡتِ وَهُمۡ يَنظُرُونَ

Likawa linabishana na wewe, ewe Nabii, kundi hilo la Waumini kuhusu kupigana baada ya kuonekana wazi kwamba hilo ni lenye kutukia, wakawa kama kwamba wao wanaongozwa kupelekwa kwenye kifo na hali wakikitazama waziwazi. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 8

وَإِذۡ يَعِدُكُمُ ٱللَّهُ إِحۡدَى ٱلطَّآئِفَتَيۡنِ أَنَّهَا لَكُمۡ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيۡرَ ذَاتِ ٱلشَّوۡكَةِ تَكُونُ لَكُمۡ وَيُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُحِقَّ ٱلۡحَقَّ بِكَلِمَٰتِهِۦ وَيَقۡطَعَ دَابِرَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na kumbukeni, enyi wabishi, ahadi ya Mwenyezi Mungu kwenu kuwa mtapata ushindi juu ya moja ya mapote mawili: msafara na bidhaa unazozibeba au jeshi la maadui, mpigane nalo na mlishinde. Na nyinyi mnapenda kupata ushindi juu ya msafara badala ya kupigana. Na Mwenyezi Mungu Anataka kuuthibitisha Uislamu na kuukuza kwa kuwaamuru nyinyi kupigana na makafiri na kuwamaliza makafiri kwa kuwaangamiza. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 8

لِيُحِقَّ ٱلۡحَقَّ وَيُبۡطِلَ ٱلۡبَٰطِلَ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Ili Mwenyezi Mungu Aupe nguvu Uislamu na watu wake na auondoe ushirikina na watu wake ingawa washirikina watalichukia hilo. info
التفاسير: