വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
32 : 39

۞ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى ٱللَّهِ وَكَذَّبَ بِٱلصِّدۡقِ إِذۡ جَآءَهُۥٓۚ أَلَيۡسَ فِي جَهَنَّمَ مَثۡوٗى لِّلۡكَٰفِرِينَ

Hakuna yoyote dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo, kwa kumnasibishia sifa isiyofaa kusifika nayo, kama vile kuwa na mshirika na mtoto, au akasema, «Mimi nimeletewa wahyi,» na hali yeye hakuletewa wahyi wa kitu chochote. Na hakuna dhalimu zaidi kuliko yule aliyeikanusha haki iliyoteremka kwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Kwani si yako huko Motoni mashukio na makazi kwa waliomkufuru Mwenyezi Mungu na wasimuamini Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie? Ndio, yako. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 39

وَٱلَّذِي جَآءَ بِٱلصِّدۡقِ وَصَدَّقَ بِهِۦٓ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُتَّقُونَ

Na yule aliyekuja na ukweli wa maneno na vitendo, miongoni mwa Manabii na wafuasi wao, na akaukubali kiimani na kivitendo, hao ndio waliokusanya sifa za uchamungu, akiwa mbele yao yule aliye mwisho wa Manabii na Mitume, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wale wenye kumuamini, wanaoifuata Sheria yake kivitendo miongoni mwa Maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie, kisha wale wenye kuja baada yao mpaka Siku ya Malipo. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 39

لَهُم مَّا يَشَآءُونَ عِندَ رَبِّهِمۡۚ ذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Wao watayapata wanayoyataka kwa Mola wao miongoni mwa aina ya vitu vya ladha na matamanio. Hayo ndiyo malipo ya anayemtii Mola wake vile inavyopasa kutiiwa na akamuabudu vile inavyopasa kuabudiwa. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 39

لِيُكَفِّرَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ أَسۡوَأَ ٱلَّذِي عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ ٱلَّذِي كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Ili Mwenyezi Mungu Awafutie yale maovu zaidi ya matendo waliyoyafanya ulimwenguni kwa sababu ya kile walichokifanya cha kurudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kutubia makosa waliyoyatenda huko, na ili Mwenyezi Mungu Awalipe mema, kwa utiifu wao ulimwenguni, malipo mazuri zaidi ya matendo ambayo walikuwa wakiyafanya, nayo ni Pepo, info
التفاسير:

external-link copy
36 : 39

أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِكَافٍ عَبۡدَهُۥۖ وَيُخَوِّفُونَكَ بِٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ

Je, kwani Mwenyezi Mungu si Mwenye kumtosheleza mja Wake Muhammad vile vitisho vya washirikina na vitimbi vyao kuwa wao hawatamfikia kwa ubaya wowote? Ndio, Yeye Atamtosheleza katika jambo la Dini yake na dunia yake, na Atamtetea dhidi ya yoyote anayemtaka kwa ubaya. Na wao wanakutisha, ewe Mtume, na waungu wao wanaodai kuwa watakudhuru. Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Ameondoa msaada Wake kwake na Akamfanya apotee njia ya haki, basi huyo hana muongozi wa kumuongoza Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 39

وَمَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن مُّضِلٍّۗ أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِعَزِيزٖ ذِي ٱنتِقَامٖ

Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Amemuafikia kumuamini Yeye na kufanya matendo yanayoambatana na Kitabu Chake na kumfuata Mtume Wake, basi huyo hana mwenye kumpoteza na kumpotosha na haki ambayo amesimama nayo. Kwani Mwenyezi Mungu si Mshindi katika kuwatesa viumbe Wake waliomkufuru na wale waliomuasi? info
التفاسير:

external-link copy
38 : 39

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۚ قُلۡ أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ إِنۡ أَرَادَنِيَ ٱللَّهُ بِضُرٍّ هَلۡ هُنَّ كَٰشِفَٰتُ ضُرِّهِۦٓ أَوۡ أَرَادَنِي بِرَحۡمَةٍ هَلۡ هُنَّ مُمۡسِكَٰتُ رَحۡمَتِهِۦۚ قُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُۖ عَلَيۡهِ يَتَوَكَّلُ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ

Na unapowauliza, ewe Mtume, hawa washirikina wanaomuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, «Ni nani aliyeziumba hizi mbingu na ardhi?» watasema, «Aliyeziumba ni Mwenyezi Mungu.» Kwa hivyo wao wanamkubali Muumba. Basi waambie, «Je, waungu hawa mnaowashirikisha na Mwenyezi Mungu wanaweza kuniepushia makero ambayo Mwenyezi Mungu Amenikadiria au kuniondolea mambo ninayoyachukia yaliyonifika? Na je, wanaweza wao kuzuia manufaa aliyonisahilishia Mwenyezi Mungu nisiyapate au kunizuilia rehema ya Mwenyezi Mungu isinifikie?» Wao watasema, «Hawawezi hilo.» Waambie, «Mwenye kunitosheleza na kuniridhisha mimi ni Mwenyezi Mungu. Kwake yeye wanategemea wenye kutegemea katika kuleta yanayowafaa na kuzuia yanayowadhuru. Yule ambaye kwenye mkono wake peke yake kuna toshelezo, Yeye Ndiye Mwenye kunitosha na Atanikifia kila linalonitia hamu. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 39

قُلۡ يَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَٰمِلٞۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Sema, ewe Mtume, uwaambie watu wako wenye ukaidi, «Fanyeni matendo kwa namna inayoridhisha nafsi zenu, kwa kuwa mmemuabudu asiyestahiki kuabudiwa na asiye na amri ya jambo lolote. Mimi ni mwenye kufanya yale niliyoamrishwa ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake katika maneno yangu na vitendo vyangu. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 39

مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيۡهِ عَذَابٞ مُّقِيمٌ

Na mtajua ni yupi atakayejiwa na adhabu yenye kumfanya mnyonge katika maisha ya ulimwenguni na atakayeshukiwa na adhabu ya daima kesho Akhera, haitamuepuka wala haitamuondokea. info
التفاسير: