വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
77 : 37

وَجَعَلۡنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلۡبَاقِينَ

Na tukawafanya watoto wa Nūḥ ndio wenye kusalia baada ya kuzamishwa watu wake. info
التفاسير:

external-link copy
78 : 37

وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ

Na tukamuwekea utajo mwema na sifa nzuri kwa watu waliokuja baada yake wakawa wanamtaja nazo. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 37

سَلَٰمٌ عَلَىٰ نُوحٖ فِي ٱلۡعَٰلَمِينَ

Amani imfikie Nūḥ na asalimike na kutajwa kwa ubaya katika kipindi cha watu wa mwisho, bali asifiwe na watu wa vizazi vinavyokuja baada yake. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 37

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Mfano wa malipo mema tuliomlipa Nūḥ, tutamlipa kila aliyefanya vizuri, miongoni mwa waja, katika kumtii Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
81 : 37

إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Hakika Nūḥ ni miongoni mwa waja wetu wenye kuamini, wenye kumtakasia Mwenyezi Mungu na wenye kufuata amri za Mwenyezi Mungu kivitendo. info
التفاسير:

external-link copy
82 : 37

ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ

Kisha tukawazamisha wengine, wenye kukanusha kati ya watu wake, kwa mafuriko, kisisalie chochote, miongoni mwao, hata jicho lenye kupepesa. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 37

۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبۡرَٰهِيمَ

Na miongoni mwa waliokuwa katika nyendo za Nūḥ, njia yake na mila yake ni Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrāhīm, info
التفاسير:

external-link copy
84 : 37

إِذۡ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلۡبٖ سَلِيمٍ

alipomjia Mola wake kwa moyo uliyojitenga na kila itikadi ya ubatilifu na tabia ya kujitukanisha, info
التفاسير:

external-link copy
85 : 37

إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَاذَا تَعۡبُدُونَ

alipomwambia babake na watu wake kwa njia ya kuwakanya, «Ni kitu gani hiko mnachokiabudu badala ya Mwenyezi Mungu? info
التفاسير:

external-link copy
86 : 37

أَئِفۡكًا ءَالِهَةٗ دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ

Je, mnataka kuabudu waungu wa kuzuliwa na mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake? info
التفاسير:

external-link copy
87 : 37

فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Mnamdhani Mola wa viumbe vyote Atawafanya nini mkimshirikisha Yeye na mkamuabudu asiyekuwa Yeye? info
التفاسير:

external-link copy
88 : 37

فَنَظَرَ نَظۡرَةٗ فِي ٱلنُّجُومِ

Akatazama mtazamo mmoja kwenye nyota kulingana na mila ya watu wake kuhusu hilo, huku akifikiria udhuru wa kuutoa ili asipate kutoka na wao kwenda kwenye sherehe zao, info
التفاسير:

external-link copy
89 : 37

فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٞ

akawaambia, «Mimi ni mgonjwa.» Hii ilikuwa ni ishara ya mbali kutoka kwake. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 37

فَتَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ مُدۡبِرِينَ

Basi wakamuacha nyuma yao. info
التفاسير:

external-link copy
91 : 37

فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمۡ فَقَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ

Akabeta kwa haraka kuelekea kwenye masanamu wa watu wake, akasema kwa njia ya kuwakejeli, «Si mkile chakula hiki ambacho washika mlango wenu wanawapatia? info
التفاسير:

external-link copy
92 : 37

مَا لَكُمۡ لَا تَنطِقُونَ

Muna nini nyinyi mbona hamsemi wala hamumjibu mwenye kuwaomba? info
التفاسير:

external-link copy
93 : 37

فَرَاغَ عَلَيۡهِمۡ ضَرۡبَۢا بِٱلۡيَمِينِ

Akawaelekea waungu wao kuwapiga na kuwavunja-vunja kwa mkono wake wa kulia, ili kuwathibitishia makosa ya kuwaabudu. info
التفاسير:

external-link copy
94 : 37

فَأَقۡبَلُوٓاْ إِلَيۡهِ يَزِفُّونَ

Wakaja kumkabili kwa haraka na mbio huku wana hasira. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 37

قَالَ أَتَعۡبُدُونَ مَا تَنۡحِتُونَ

Ibrāhīm akakutana na wao akiwa imara kwa kusema, «Vipi mtaabudu masanamu mnaowachonga nyinyi wenyewe na mnaowatengeneza kwa mikono yenu, info
التفاسير:

external-link copy
96 : 37

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ وَمَا تَعۡمَلُونَ

na mnaacha kumuabudu Mola wenu Aliyewaumba nyinyi na Akayaumba matendo yenu?» info
التفاسير:

external-link copy
97 : 37

قَالُواْ ٱبۡنُواْ لَهُۥ بُنۡيَٰنٗا فَأَلۡقُوهُ فِي ٱلۡجَحِيمِ

Hoja ilipowasimamia, waliamua kutumia nguvu na wakasema, «Jengeni jengo kwa ajili yake, mlijaze kuni kisha mumtupe ndani yake» info
التفاسير:

external-link copy
98 : 37

فَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدٗا فَجَعَلۡنَٰهُمُ ٱلۡأَسۡفَلِينَ

Watu wa Ibrāhīm wakataka kumfanyia vitimbi ili wamuangamize, tukawafanya wao kuwa ndio wenye kutendeshwa nguvu na kushindwa. Mwenyezi Mungu Akavirudisha vitimbi vyao kwenye shingo zao na akaufanya ule moto uwe baridi na salama kwa Ibrāhīm. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 37

وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهۡدِينِ

Akasema Ibrāhīm, «Mimi nahamia kwa Mola wangu kutoka kwenye mji wa watu wangu kuelekea pale ambapo nitamakinika kumuabudu Mola wangu, kwani Yeye Atanielekeza kwenye kheri ya Dini yangu na dunia yangu. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 37

رَبِّ هَبۡ لِي مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Mola wangu! Nipe mtoto mwema.» info
التفاسير:

external-link copy
101 : 37

فَبَشَّرۡنَٰهُ بِغُلَٰمٍ حَلِيمٖ

Tukamkubalia ombi lake na tukambashiria kuwa atapata mtoto wa kiume atakayekuwa mpole ukubwani mwake, naye ni Ismā'īl. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 37

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعۡيَ قَالَ يَٰبُنَيَّ إِنِّيٓ أَرَىٰ فِي ٱلۡمَنَامِ أَنِّيٓ أَذۡبَحُكَ فَٱنظُرۡ مَاذَا تَرَىٰۚ قَالَ يَٰٓأَبَتِ ٱفۡعَلۡ مَا تُؤۡمَرُۖ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Alipokuwa mkubwa Ismā'īl, akawa anatembea na babake, babake alimwambia, «Mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja, je, una maoni gani?» (na ndoto za Manabii ni za kweli). Ismā'īl akasema, kwa kumridhisha Mola wake, kumtii mzazi wake na kumsaidia juu ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, «Endelea katika jambo Alilokuamrisha Mwenyezi Mungu la kunichinja mimi. Utanikuta, Mwenyezi Mungu Akitaka, ni mvumilivu, mtiifu na ni mwenye kutarajia malipo mema (kutoka kwa Mwenyezi Mungu)». info
التفاسير: