വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

Ar-Rum

external-link copy
1 : 30

الٓمٓ

«Alif, Lām, Mīm» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa- katwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 30

غُلِبَتِ ٱلرُّومُ

Wafursi waliwashinda Warumi info
التفاسير:

external-link copy
3 : 30

فِيٓ أَدۡنَى ٱلۡأَرۡضِ وَهُم مِّنۢ بَعۡدِ غَلَبِهِمۡ سَيَغۡلِبُونَ

katika sehemu za karibu za ardhi ya Shamu kuelekea Uajemi. Na Warumi watawashinda Wafursi info
التفاسير:

external-link copy
4 : 30

فِي بِضۡعِ سِنِينَۗ لِلَّهِ ٱلۡأَمۡرُ مِن قَبۡلُ وَمِنۢ بَعۡدُۚ وَيَوۡمَئِذٖ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

katika kipindi kisichopita miaka kumi na kisichopungua miaka mitatu. Ni ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, amri yote kabla ya ushindi wa Warumi na baada yake. Na siku hiyo ambayo Warumi watapata ushindi juu ya Wafursi Waumini wataifurahia nusura ya Mwenyezi Mungu kwa Warumi juu ya Wafursi. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 30

بِنَصۡرِ ٱللَّهِۚ يَنصُرُ مَن يَشَآءُۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Na Mwenyezi Mungu, Kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anamsaidia Anayemtaka na Anaacha kumsaidia Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Mshindi Ambaye hakuna wa kushindana naye, Ndiye Mwenye kumrehemu Anayemtaka miongoni mwa viumbe Vyake. Na hilo lilithibitika, na Warumi waliwashinda Wafursi baada ya miaka saba, na Waislamu wakafurahi kwa hilo, kwa kuwa Warumi walikuwa ni watu wa Kitabu ingawa wamekipotosha. info
التفاسير: