വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
92 : 3

لَن تَنَالُواْ ٱلۡبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ

Hamuwezi kupata Pepo ng’o! mpaka mtoe sadaka katika vile vitu mnavyovipenda. Na chochote mnachokitoa sadaka, kiwe ni kichache au ni kingi, basi Mwenyezi Mungu Anakijua mno na Atamlipa kila mtoaji malipo yanayolingana na kitendo chake. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 3

۞ كُلُّ ٱلطَّعَامِ كَانَ حِلّٗا لِّبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسۡرَٰٓءِيلُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ مِن قَبۡلِ أَن تُنَزَّلَ ٱلتَّوۡرَىٰةُۚ قُلۡ فَأۡتُواْ بِٱلتَّوۡرَىٰةِ فَٱتۡلُوهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Vyakula vyote vizuri vilikuwa ni halali kwa wana wa Ya'qūb, amani imshukiye, isipokuwa vile ambavyo Ya’qūb alijiharamishia yeye mwenyewe kwa sababu ya ugonjwa uliompata. Na hayo yalikuwa kabla ya Taurati haijateremshwa. Taurati ilipoteremshwa, Mwenyezi Mungu Aliwaharamishia Wana wa Isrāīl baadhi ya vyakula vilivyokuwa halali kwao. Na hilo ni kwa sababu ya dhuluma zao na uovu wao. Waambie, ewe Mtume, «Ileteni Taurati na muyasome yaliyomo ndani yake iwapo muna hakika ya madai yenu kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha humo uharamu wa aliojiharamishia Ya'qūb nafsi yake, ili mpate kuujua ukweli wa yale yaliyokuja katika Qur’ani ya kwamba Mwenyezi Mungu Hakuwaharamishia Wana wa Isrāīl chochote kabla ya kuteremka Taurati, isipokuwa yale ambayo Ya'qūb alijiharamishia nafsi yake. info
التفاسير:

external-link copy
94 : 3

فَمَنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Basi yule atakayemzulia Mwenyezi Mungu urongo baada ya kuisoma Taurati na ukweli kuwa wazi, basi hao ndio madhalimu wanaomzulia Mwenyezi Mungu ya batili. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 3

قُلۡ صَدَقَ ٱللَّهُۗ فَٱتَّبِعُواْ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Waambie, ewe Mtume, Mwenyezi Mungu Amesema kweli katika Aliyoyatolea habari na yale ya Sheria Aliyoipitisha. Basi iwapo nyinyi ni wakweli katika mahaba yenu na kujinasibisha kwenu na rafiki halisi wa Mwenyezi Mungu, Ibrāhīm, amani imshukiye, fuateni mila yake Aliyoipitisha Mwenyezi Mungu kupitia kwa ulimi wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Kwani hiyo ndiyo haki isiyokuwa na shaka. Na wala hakuwa Ibrāhīm, amani imshukie, ni kati ya wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, katika kumpwekesha na kumuabudu, na yoyote. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 3

إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٖ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكٗا وَهُدٗى لِّلۡعَٰلَمِينَ

Hakika nyumba ya mwanzo iliyojengwa kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu ni hiyo nyumba ya Mwenyezi Mungu takatifu iliyoko Maka. Na nyumba hiyo imebarikiwa, mema huko huongezwa na rehema huko hushuka. Na katika kuielekea nyumba hiyo kwenye Swala na kuiendea kipindi cha kutekeleza Hija na Umra, pana wema na uongofu kwa watu wote. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 3

فِيهِ ءَايَٰتُۢ بَيِّنَٰتٞ مَّقَامُ إِبۡرَٰهِيمَۖ وَمَن دَخَلَهُۥ كَانَ ءَامِنٗاۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلٗاۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Katika Nyumba hii kuna alama waziwazi ya kwamba hiyo ni katika ujenzi wa Ibrāhīm na kwamba Mwenyezi Mungu ameitukuza na kuipa heshima. Kati ya alama hizo ni Maqām ya Ibrāhīm, amani imshukie, nayo ni lile jiwe ambalo alikuwa akisimama juu yake wakati alipokuwa akiziinua nguzo za Alkaba, yeye na mwanawe Ismā'īl. Na yoyote mwenye kuingia Nyumba hii atapata amani ya nafsi yake, hapana yoyote atakayemkusudia kwa uovu. Na Mwenyezi Mungu Amewajibisha kwa mwenye uwezo katika watu, popote atakapokuwa kuiendea nyumba hii ili kutekeleza matendo ya Hija. Na yoyote mwenye kuikanusha faradhi ya Hija, basi huyo amekufuru. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi naye, Hana haja ya hija yake wala amali yake na wala Hana haja na viumbe vyake vyote. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 3

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعۡمَلُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliepewa vitabu kati ya Mayahudi na Wanaswara, «Kwa nini mnazikanusha hoja za Mwenyezi Mungu zinazojulisha kwamba dini ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu na mnayakanusha yaliyomo kwenye vitabu vyenu miongoni mwa dalili na hoja juu ya hilo hali ya kuwa nyinyi mnajua? Na Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya kitendo chenu mnachokifanya.» Katika haya, pana makemeo na ahadi ya adhabu kwao. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 3

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ تَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَأَنتُمۡ شُهَدَآءُۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia Mayahudi na Wanaswara, «Mbona mnamzuia kuingia katika Uislamu yule mtu atakaye hivyo na mnamtakia upotofu na kupinduka kwenye lengo na muelekeo wa kisawa, na nyinyi mnajua kwamba niliyokuja nayo ndiyo haki?» Basi, Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika kwa mnayoyatenda, na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 3

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تُطِيعُواْ فَرِيقٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَرُدُّوكُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡ كَٰفِرِينَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazitumia Sheria Zake kwa kuzifuata, iwapo mtalitii kundi la Mayahudi na Wanaswara, miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu Amewapa Taurati na Injili, watawapoteza na watawatia shaka katika dini yenu, ili mupate kurudi nyuma na kuikanusha haki baada ya kuwa mlikuwa waumini wa haki hiyo, basi msiwaamini juu ya dini yenu wala msiwakubalie rai yoyote au shauri. info
التفاسير: