വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

Al-Furqan

external-link copy
1 : 25

تَبَارَكَ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡفُرۡقَانَ عَلَىٰ عَبۡدِهِۦ لِيَكُونَ لِلۡعَٰلَمِينَ نَذِيرًا

Ni kubwa mno baraka za Mwenyezi Mungu na ni mengi sana mema Yake na ni kamilifu sifa Zake, Aliyetakasika na kutukuka, Ambaye Ameiteremsha Qur’ani, yenye kupambanua baina ya ukweli na ubatilifu, kwa mja Wake Muhammad, rehemea ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili awe ni mjumbe kwa binadamu na majini na awe muonyaji wa adhabu ya Mwenyezi Mungu kwao. info
التفاسير: