വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
37 : 24

رِجَالٞ لَّا تُلۡهِيهِمۡ تِجَٰرَةٞ وَلَا بَيۡعٌ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَإِقَامِ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءِ ٱلزَّكَوٰةِ يَخَافُونَ يَوۡمٗا تَتَقَلَّبُ فِيهِ ٱلۡقُلُوبُ وَٱلۡأَبۡصَٰرُ

Wanaume ambao hawapumbazwi na ununuzi wala uuzaji na jambo la kumtaja Mwenyezi Mungu, kusimamisha Swala na kutoa Zaka kwa anayestahiki kupewa; wanaiogopa Siku ya Kiyama ambayo nyoyo zinageukageuka baina ya matumaini ya kuokoka na kicho cha kuangamia, na macho yatakuwa yanageukageuka yanatazama ni mwisho gani yataishia? info
التفاسير:

external-link copy
38 : 24

لِيَجۡزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحۡسَنَ مَا عَمِلُواْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضۡلِهِۦۗ وَٱللَّهُ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ

Ili Mwenyezi Mungu Awape malipo mema ya matendo yao mazuri zaidi na Awaongezee kutokana na wema Wake. Na Mwenyezi Mungu Anamruzuku Anayemtaka bila kumhesabia, bali Anampa malipo ambayo matendo yake mema hayakuyafikia, na pasi na hesabu wala kipimo. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 24

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَعۡمَٰلُهُمۡ كَسَرَابِۭ بِقِيعَةٖ يَحۡسَبُهُ ٱلظَّمۡـَٔانُ مَآءً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَهُۥ لَمۡ يَجِدۡهُ شَيۡـٔٗا وَوَجَدَ ٱللَّهَ عِندَهُۥ فَوَفَّىٰهُ حِسَابَهُۥۗ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Na wale waliomkanusha Mola wao na wakawafanya warongo Mitume Wake, matendo yao waliyoyategemea kuwa yatawafaa huko Akhera, kama kuunga kizazi, kuwaacha huru mateka na yasiyokuwa hayo, yatakuwa ni kama mangati, nayo ni yale yanayoonekana kama maji juu ya ardhi tambarare kipindi cha mchana cha jua kali, mwenye kiu akiyaona anadhani ni maji, na akiyajia hakuti kuwa ni maji. Basi kafiri anadhani kwamba matendo yake yatamfaa, na ifikapo Siku ya Kiyama atakuta kuwa hayana malipo mema, na hapo atamkuta Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Anamngojea Ampe malipo ya matendo yake kikamilifu. Na Mwenyezi Mungu ni Mpesi wa kuhesabu. Basi wajinga wasione kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu imekawia kuwa, kwani hiyo hapana budi kuja kwake. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 24

أَوۡ كَظُلُمَٰتٖ فِي بَحۡرٖ لُّجِّيّٖ يَغۡشَىٰهُ مَوۡجٞ مِّن فَوۡقِهِۦ مَوۡجٞ مِّن فَوۡقِهِۦ سَحَابٞۚ ظُلُمَٰتُۢ بَعۡضُهَا فَوۡقَ بَعۡضٍ إِذَآ أَخۡرَجَ يَدَهُۥ لَمۡ يَكَدۡ يَرَىٰهَاۗ وَمَن لَّمۡ يَجۡعَلِ ٱللَّهُ لَهُۥ نُورٗا فَمَا لَهُۥ مِن نُّورٍ

Au matendo yao yawe mfano wa giza ndani ya bahari yenye kina, juu yake kuna mawimbi, na juu ya mawimbi kuna mawimbi mengine, na juu ya mawimbi hayo kuna mawingu mazito. Hilo ni giza kubwa sana, giza juu ya giza, pindi atowapo mkono wake mtazamaji, kamwe hakaribii kuuona kwa ukubwa wa giza. Limerundikana kwa makafiri giza la ushirikina, upotevu na uharibifu wa matendo. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu Hakumpatia nuru itokamanayo na Kitabu Chake na mwendo wa Mtume Wake, basi huyo hana wa kumuongoza. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 24

أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُسَبِّحُ لَهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱلطَّيۡرُ صَٰٓفَّٰتٖۖ كُلّٞ قَدۡ عَلِمَ صَلَاتَهُۥ وَتَسۡبِيحَهُۥۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ

Kwani hukujua, ewe Mtume, kwamba Mwenyezi Mungu vinamtakasa Yeye viumbe vilivyoko mbinguni na ardhini. Na ndege wamezikunjua mbawa zao huko juu angani wanamtakasa Mola wao? Kila kiumbe, Mwenyezi Mungu Amemfundisha namna ya kumswalia na ya kumtakasa. Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Anayaona anayoyafanya kila mwenye kuabudu na kutakasa, hakuna chochote kinachofichika Kwake Yeye kuhusu hayo, na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 24

وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلۡمَصِيرُ

Ni wa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, ufalme wa mbinguni na ardhini. Ndiye Mwenye utawala wa hizo zote. Na Kwake Yeye ndio marejeo Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 24

أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُزۡجِي سَحَابٗا ثُمَّ يُؤَلِّفُ بَيۡنَهُۥ ثُمَّ يَجۡعَلُهُۥ رُكَامٗا فَتَرَى ٱلۡوَدۡقَ يَخۡرُجُ مِنۡ خِلَٰلِهِۦ وَيُنَزِّلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن جِبَالٖ فِيهَا مِنۢ بَرَدٖ فَيُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ وَيَصۡرِفُهُۥ عَن مَّن يَشَآءُۖ يَكَادُ سَنَا بَرۡقِهِۦ يَذۡهَبُ بِٱلۡأَبۡصَٰرِ

Kwani hukuona kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kutukuka, Anayapeleka mawingu pale Anapopataka, kisha Anayakusanya baada ya kuwa mbalimbali, kisha anayafanya yapandane na yarundikane, kisha Anaiteremshe mvua kutoka kwenye mrundiko huo? Na Anateremsha, kutoka kwenye mawingu yanayofanana na milima ya mawe kwa ukubwa wake, mvua ya barafu, Akaipeleka kwa amtakaye kati ya waja Wake na Akaiyondosha kwa Amtakaye kati yao kuambatana na hekima Yake na mpango Wake. Unakaribia mwangaza wa umeme huo umemetekao huko mawinguni, kwa ukali wake, kuyapofua macho ya wenye kuutazama. info
التفاسير: