വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

Al-Hajj

external-link copy
1 : 22

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡۚ إِنَّ زَلۡزَلَةَ ٱلسَّاعَةِ شَيۡءٌ عَظِيمٞ

Enyi watu! Tahadharini na mateso ya Mwenyezi Mungu, kwa kufuata amri zake na kuepuka makatazo yake, kwani vituko vitakavyotokea pindi kisimamapo Kiyama na mtetemeko mkubwa wa ardhi utakaofanya pambizo zake zipasukepasuke, ni jambo kubwa ambalo hakuna mwenye kulikadiria wala kulifikia vile litakavyokuwa, wala kujua namna yake isipokua Mola wa viumbe wote. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 22

يَوۡمَ تَرَوۡنَهَا تَذۡهَلُ كُلُّ مُرۡضِعَةٍ عَمَّآ أَرۡضَعَتۡ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمۡلٍ حَمۡلَهَا وَتَرَى ٱلنَّاسَ سُكَٰرَىٰ وَمَا هُم بِسُكَٰرَىٰ وَلَٰكِنَّ عَذَابَ ٱللَّهِ شَدِيدٞ

Siku mtakapokiona Kiyama kimesima, mama atamsahau mtoto wake mchanga aliyempa titi lake kunyoya kwa shida iliyomshukia, mwenye mimba ataharibu mimba yake kwa babaiko na akili za watu zitapotea watakuwa ni kama walevi kwa tukio hilo kubwa na babaiko na hali wao si walevi wa pombe, lakini ni ukali wa adhabu ndio uliowapoteza akili zao na hisia zao. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 22

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِي ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيۡطَٰنٖ مَّرِيدٖ

Na baadhi ya vichwa vya ukafiri miongoni mwa watu wanaleta utesi na wanatilia shaka uweza wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, kwa ujinga wao wa kutojua uhakika wa uweza huu na kwa kumfuata kila shetani mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mitume Wake kati ya viongozi wa upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 22

كُتِبَ عَلَيۡهِ أَنَّهُۥ مَن تَوَلَّاهُ فَأَنَّهُۥ يُضِلُّهُۥ وَيَهۡدِيهِ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ

Mwenyezi Mungu amehukumu na kukadiria juu ya huyu Shetani kwamba yeye ampoteze kila mwenye kumfuata na asimuongoze kwenye ukweli, bali amuandamishe njia ya kupelekea kwenye adhabu ya Jahanamu uliowashwa, ikiwa ni malipo ya kumfuata kwake huyo Shetani. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 22

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي رَيۡبٖ مِّنَ ٱلۡبَعۡثِ فَإِنَّا خَلَقۡنَٰكُم مِّن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ مِنۡ عَلَقَةٖ ثُمَّ مِن مُّضۡغَةٖ مُّخَلَّقَةٖ وَغَيۡرِ مُخَلَّقَةٖ لِّنُبَيِّنَ لَكُمۡۚ وَنُقِرُّ فِي ٱلۡأَرۡحَامِ مَا نَشَآءُ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى ثُمَّ نُخۡرِجُكُمۡ طِفۡلٗا ثُمَّ لِتَبۡلُغُوٓاْ أَشُدَّكُمۡۖ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَيۡلَا يَعۡلَمَ مِنۢ بَعۡدِ عِلۡمٖ شَيۡـٔٗاۚ وَتَرَى ٱلۡأَرۡضَ هَامِدَةٗ فَإِذَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡهَا ٱلۡمَآءَ ٱهۡتَزَّتۡ وَرَبَتۡ وَأَنۢبَتَتۡ مِن كُلِّ زَوۡجِۭ بَهِيجٖ

Enyi watu, mkiwa muna shaka ya kuwa Mwenyzi Mungu atawafufua wafu, basi sisi tumemuumba baba yenu Adam kutokana na mchanga kisha kizazi chake kikazaana kutokana na nutfah, nayo ni manii ambayo mwanamume anayarusha kwenye uzao wa mwnamke, yakageuka kwa uweza wa Mwenyezi Mungu yakawa 'alaqah, nalo ni pande la damu nyekundu iliyo nzito, kisha yakawa mudghah, nacho ni kinofu kidogo cha nyama cha kuweza kutafunika, mara nyingine kikawa kitaumbwa, yaani kiumbike kikamilifu mpaka kifikiye hadi ya kutoka kwa mtoto akiwa hai, na mara nyingine kisiumbike kikamilifu kikatoka kabla ya kutimia, ili tuwafafanulie ukamilifu wa uweza wetu wa kupelekesha miongo ya uumbaji. Na tunakibakisha kwenye zao tunachokitaka, nacho ni kile kinachoendelezwa kuumbwa kwake mpaka wakati wa kuzaliwa kwake na itimie ile miongo ya kuzaliwa wana wa matumboni wakiwa wadogo, wakuwe mpaka wafikie umri wa kuwa na nguvu, nao ni wakati wa ubarobaro na nguvu na kukamilika akili. Na baadhi ya watoto huenda wakafa kabla ya hapo, na baadhi yao wanakuwa mpaka wanafikisha miaka ya ukongwe na udhaifu wa akili, akawa huyu aliyezeeka hajui kitu alichokuwa akikijua kabla ya hapo. Na utaiyona ardhi ni kavu, imekufa haina mimea yoyote, tuyateremshapo maji juu yake, inatikisika kwa mimea ikawa inafunguka, inachepuza, inanyanyuka na kuongezeka kwa kutosheka na maji na ikaotesha kila aina ya mimea mizuri yenye kuwafurahisha wenye kuangalia. info
التفاسير: