വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
98 : 18

قَالَ هَٰذَا رَحۡمَةٞ مِّن رَّبِّيۖ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ رَبِّي جَعَلَهُۥ دَكَّآءَۖ وَكَانَ وَعۡدُ رَبِّي حَقّٗا

Dhulqarnain akasema, «Hiki nilichokijenga cha kuzuia uharibifu wa Ya’jūj na Ma’jūj ni rehema kwa watu itokayo kwa Mola wangu, na ahadi ya Mwenyezi Mungu itakapokuja ya kutoka Ya’jūj na Ma’jūj, Atakifanya kigongeke- gongeke kivunjike na kiwe sawa na ardhi, na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli.» info
التفاسير:

external-link copy
99 : 18

۞ وَتَرَكۡنَا بَعۡضَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ يَمُوجُ فِي بَعۡضٖۖ وَنُفِخَ فِي ٱلصُّورِ فَجَمَعۡنَٰهُمۡ جَمۡعٗا

Na tutawaacha Ya’jūj na Ma’jūj, siku ya kuwajia ahadi yetu, watangamane wao kwa wao na wachanganyike kwa wingi wao, na Pembe ya Ufufuzi itapulizwa na tutawakusanya viumbe wote ili wahesabiwe na walipwe. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 18

وَعَرَضۡنَا جَهَنَّمَ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡكَٰفِرِينَ عَرۡضًا

Na tutauhudhurisha moto wa Jahanamu kwa makafiri na tutaudhihirisha kwao waushuhudie, ili tuwaoneshe ubaya wa mwisho wao. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 18

ٱلَّذِينَ كَانَتۡ أَعۡيُنُهُمۡ فِي غِطَآءٍ عَن ذِكۡرِي وَكَانُواْ لَا يَسۡتَطِيعُونَ سَمۡعًا

Wale ambao macho yao ulimwenguni yalikuwa yamefinikwa na kutonikumbuka, hayazioni dalili zangu, na walikuwa hawawezi kustahamili kuzisikia hoja zangu zenye kupelekea kuniamini mimi na Mtume wangu. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 18

أَفَحَسِبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَن يَتَّخِذُواْ عِبَادِي مِن دُونِيٓ أَوۡلِيَآءَۚ إِنَّآ أَعۡتَدۡنَا جَهَنَّمَ لِلۡكَٰفِرِينَ نُزُلٗا

Je, walidhani walionikanusha kuwa watawafanya waja wangu kuwa ni waungu badala yangu, wawe ni wategemewa wao? Kwa hakika tumewatayarishia wenye kukanusha moto wa Jahanamu uwe ndio mashukio yao. info
التفاسير:

external-link copy
103 : 18

قُلۡ هَلۡ نُنَبِّئُكُم بِٱلۡأَخۡسَرِينَ أَعۡمَٰلًا

Waambie watu, ewe Mtume, kwa kuwaonya: Je, tuwapashe habari ya watu wenye vitendo vya hasara zaidi? info
التفاسير:

external-link copy
104 : 18

ٱلَّذِينَ ضَلَّ سَعۡيُهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُمۡ يَحۡسَبُونَ أَنَّهُمۡ يُحۡسِنُونَ صُنۡعًا

Wao ni wale ambao matendo yao yalipotea katika maisha ya ulimwengu- nao ni washirikina wa watu wako na wengineo kati ya wale waliopotea njia ya sawa wasiwe kwenye uongofu wala usawa- na hali wao wanadhania kuwa wanayatengeneza matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
105 : 18

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ وَلِقَآئِهِۦ فَحَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَلَا نُقِيمُ لَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَزۡنٗا

Hao ndio waliopata hasara zaidi kivitendo, ndio wao waliozikataa aya za Mola wao na wakazikanusha na wakapinga kuwa watakutana na Yeye Siku ya Kiyama, hivyo basi matendo yao yakabatilika kwa sababu ya ukafiri wao na kwa hivyo hatutawajali chochote Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
106 : 18

ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُمۡ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُواْ وَٱتَّخَذُوٓاْ ءَايَٰتِي وَرُسُلِي هُزُوًا

Malipo hayo waliyoandaliwa kwa kubatilika matendo yao, ni moto wa Jahanamu, kwa sababu ya kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu na kuzifanyia kwao shere na mchezo aya Zake na hoja za Mitume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
107 : 18

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ كَانَتۡ لَهُمۡ جَنَّٰتُ ٱلۡفِرۡدَوۡسِ نُزُلًا

Hakika wale walioniamini, wakawakubali Mitume wangu na wakafanya mema watapata Pepo ya juu kabisa, ya kati na kati na yenye mashukio bora kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 18

خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يَبۡغُونَ عَنۡهَا حِوَلٗا

Hali ya kukaa milele humo, hawatataka kuepukana nayo kwa kuwa na hamu nayo na kuipenda. info
التفاسير:

external-link copy
109 : 18

قُل لَّوۡ كَانَ ٱلۡبَحۡرُ مِدَادٗا لِّكَلِمَٰتِ رَبِّي لَنَفِدَ ٱلۡبَحۡرُ قَبۡلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَٰتُ رَبِّي وَلَوۡ جِئۡنَا بِمِثۡلِهِۦ مَدَدٗا

Sema, ewe Mtuume, «Lau maji ya bahari yalikuwa wino wa kalamu za kuandikia maneno ya Mwenyezi Mungu yanayokusanya elimu Yake, hukumu Zake na yale Aliyowatumia wahyi Malaika Wake na Mitume Wake, yangaliisha maji ya bahari kabla maneno ya Mwenyezi Mungu hayajaisha, hata kama tulikuja na bahari nyingine za kuongezea mfano wa bahari hiyo. Katika aya hii pana kuthibitisha kikweli sifa ya kusema kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama kunakonasibiana na utkufu Wake na ukamilifu Wake.» info
التفاسير:

external-link copy
110 : 18

قُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ يُوحَىٰٓ إِلَيَّ أَنَّمَآ إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ فَمَن كَانَ يَرۡجُواْ لِقَآءَ رَبِّهِۦ فَلۡيَعۡمَلۡ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَلَا يُشۡرِكۡ بِعِبَادَةِ رَبِّهِۦٓ أَحَدَۢا

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Kwa kweli, mimi ni binadamu kama nyinyi, ninaletewa wahyi kutoka kwa Mola wangu kwamba mola wenu ni Mola Mmoja. Basi yoyote anayekuwa ni mwenye kuiyogopa adhabu ya Mola wake na ana matumaini kupata malipo yake mazuri Siku ya Kiyama, na atende matendo mema kwa ajili ya Mola wake yenye kuafikiana na sheria Yake, na asimshirikishe yoyote pamoja na Yeye katika ibada.» info
التفاسير: