വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
32 : 15

قَالَ يَٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Mwenyezi Mungu Akasema kumwambia Iblisi, «Una nini wewe kutosujudu pamoja na Malaika?» info
التفاسير:

external-link copy
33 : 15

قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُۥ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ

Iblisi akasema akionyesha kiburi chake na uhasidi wake, «Hainasibiani na mimi nimsujudie mtu uliyempatisha kutokana na udongo mkavu, uliokuwa mweusi na uliogeuka.» info
التفاسير:

external-link copy
34 : 15

قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akamwambia, «Basi toka Peponi, wewe ushafukuzwa na umeepushwa na kila jema, info
التفاسير:

external-link copy
35 : 15

وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

umeshukiwa na laana na umewekwa mbali na rehema yangu mpaka Siku ya kufufuliwa watu ili wahesabiwe na walipwe..» info
التفاسير:

external-link copy
36 : 15

قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Iblisi akasema, «Ewe Mola wangu! Nipatie muda mpaka siku ya wewe kuwafufua waja wako , nayo ni Siku ya Kiyama.» info
التفاسير:

external-link copy
37 : 15

قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

Mwenyezi Mungu Akamwambia, «Wewe ni miongoni mwa wale niliowapa muda na kuchelewesha kuwaangamiza mpaka siku ambayo viumbe wote watakufa baada ya Mpulizo wa kwanza, info
التفاسير:

external-link copy
38 : 15

إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ

na siyo mpaka siku ya Ufufuzi. Na alikubaliwa hilo kwa njia ya kulegezewa na kuachiliwa, na ni mtihani kwa binadamu na majini. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 15

قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Akasema Iblisi, «Mola wangu, kwa sababu ya vile ulivyonipoteza na kunipotosha nitawapambia vizazi vya Ādam kukuasi katika ardhi na nitawapoteza wote wasiione njia ya uongofu, info
التفاسير:

external-link copy
40 : 15

إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ

isipokuwa waja wako ambao umewaongoa wakakutakasia ibada peke yako pasi na viumbe wako wengine.» info
التفاسير:

external-link copy
41 : 15

قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَيَّ مُسۡتَقِيمٌ

Akasema Mwenyezi Mungu , «Hii ni njia nyofu iliyolingana inayofikisha kwangu na kwenye Nyumba ya ukarimu wangu. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 15

إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ

Kwa kweli, wale waja wangu ambao wamenitakasia mimi sitakupatia uwezo juu ya nyoyo zao ili uwapoteze kwa uwezo huo na njia iliyonyoka. Lakini uwezo wako utakuwa ni juu ya yule aliyekuandama miongoni mwa wapotofu washirikina ambao wameukubali usimamizi wako na kukutii badala ya kunitii mimi.» info
التفاسير:

external-link copy
43 : 15

وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Hakika Moto mkali ndio agizo la Iblisi na wafuasi wake wote. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 15

لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٰبٖ لِّكُلِّ بَابٖ مِّنۡهُمۡ جُزۡءٞ مَّقۡسُومٌ

Una milango saba , kila mlango uko chini ya mwengine. Kila mlango utakuwa na fungu na sehemu la wafuasi wa Iblisi kulingana na matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 15

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ

Hakika wale waliomcha Mwenyezi Mungu, kwa kuyafuata Aliyoyaamrisha na kujiepusha na aliyoyakataza.watakuwa kwenye mabustani ya Pepo na mito ipitayo. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 15

ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ

Wataambiwa, «Ingieni Mabustani haya mkiwa watulivu mumesalimika na kila ovu mumeaminika na kila adhabu. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 15

وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ

Na tutawaondolea yaliyomo ndani ya nyoyo zao ya chuki na uadui, wataishi Peponi wakiwa ndugu wapendanao, watakaa kwenye vitanda vikubwa na nyuso zao zitaelekeana katika hali ya kuungana na kupendana. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 15

لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبٞ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ

Haitawapata humo tabu wala uchovu. Na wao ni wenye kusalia humo milele. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 15

۞ نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Wapashe habari, ewe Mtume, waja wangu kwamba mimi ni mwenye kuwasamehe Waumini wenye kutubia, ni mwenye huruma kwao, info
التفاسير:

external-link copy
50 : 15

وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ ٱلۡعَذَابُ ٱلۡأَلِيمُ

na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iumizayo yenye kutia uchungu kwa wasiotubia. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 15

وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ

Na wapashe habari, ewe Mtume, kuhusu wageni wa Ibrāhīm miongoni mwa Malaika ambao walimpa habari njema za kupata mwana na za kuangamia kwa jamaa za Lūṭ. info
التفاسير: