വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - അബ്ദുല്ലാഹ് മുഹമ്മദ് & നാസ്വിർ ഖമീസ്.

Al-Masad

external-link copy
1 : 111

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٖ وَتَبَّ

Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutu. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 111

مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ

Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukia. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 111

سَيَصۡلَىٰ نَارٗا ذَاتَ لَهَبٖ

Ataingia kwenye Moto wenye kuroroma, info
التفاسير:

external-link copy
4 : 111

وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ

yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 111

فِي جِيدِهَا حَبۡلٞ مِّن مَّسَدِۭ

Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini. info
التفاسير: