ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ರುವ್ವಾದ್ ಅನುವಾದ ಕೇಂದ್ರ

ಪುಟ ಸಂಖ್ಯೆ:close

external-link copy
197 : 2

ٱلۡحَجُّ أَشۡهُرٞ مَّعۡلُومَٰتٞۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ ٱلۡحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي ٱلۡحَجِّۗ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ يَعۡلَمۡهُ ٱللَّهُۗ وَتَزَوَّدُواْ فَإِنَّ خَيۡرَ ٱلزَّادِ ٱلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُونِ يَٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Hija ni miezi maalumu. Basi anayehirimia Hija ndani yake (miezi hiyo), basi asijamiiane wala asipindukie mipaka wala asibishane katika Hija. Na chochote mnachokifanya katika heri, Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu. Na hakika, masurufu (yaliyo) bora zaidi ni ucha Mungu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili ya hali ya juu! info
التفاسير:

external-link copy
198 : 2

لَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَبۡتَغُواْ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكُمۡۚ فَإِذَآ أَفَضۡتُم مِّنۡ عَرَفَٰتٖ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ عِندَ ٱلۡمَشۡعَرِ ٱلۡحَرَامِۖ وَٱذۡكُرُوهُ كَمَا هَدَىٰكُمۡ وَإِن كُنتُم مِّن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلضَّآلِّينَ

Hakuna ubaya wowote juu yenu kutafuta fadhila kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi mtakapomiminika kutoka 'Arafat, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril Haram (eneo takatifu). Na mtajeni kama alivyowaongoa, ijapokuwa kabla ya hilo mlikuwa miongoni mwa waliopotea. info
التفاسير:

external-link copy
199 : 2

ثُمَّ أَفِيضُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَفَاضَ ٱلنَّاسُ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. info
التفاسير:

external-link copy
200 : 2

فَإِذَا قَضَيۡتُم مَّنَٰسِكَكُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَذِكۡرِكُمۡ ءَابَآءَكُمۡ أَوۡ أَشَدَّ ذِكۡرٗاۗ فَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا وَمَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖ

Na mkishatimiza ibada zenu za Hija, mtajeni Mwenyezi Mungu kama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu au utajo mkubwa zaidi. Na katika watu kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani!” Naye katika Akhera hana fungu lolote. info
التفاسير:

external-link copy
201 : 2

وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَآ ءَاتِنَا فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ حَسَنَةٗ وَقِنَا عَذَابَ ٱلنَّارِ

Na miongoni mwao kuna wale wanaosema, “Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde kutokana na adhabu ya Moto!” info
التفاسير:

external-link copy
202 : 2

أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ نَصِيبٞ مِّمَّا كَسَبُواْۚ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Hao ndio walio na fungu kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. info
التفاسير: