ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ಅಲಿ ಮುಹ್ಸಿನ್ ಅಲ್-ಬರ್ವಾನಿ

external-link copy
35 : 28

قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجۡعَلُ لَكُمَا سُلۡطَٰنٗا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيۡكُمَا بِـَٔايَٰتِنَآۚ أَنتُمَا وَمَنِ ٱتَّبَعَكُمَا ٱلۡغَٰلِبُونَ

(Mwenyezi Mungu) akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa nduguyo, na tutakupeni madaraka, hata wasikufikilieni. Kwa sababu ya Ishara zetu nyinyi na watakao kufuateni mtashinda. info

Mwenyezi Mungu akasema, kuitikia ombi lake: Tutakutia nguvu kwa kumtuma Harun. Na tutakupeni nyinyi wawili madaraka, na tutakuungeni mkono kwa miujiza. Kwa hivyo hawatoweza kukuvamieni. Na nyinyi wawili na walio kufuateni na wakaongoka kwa msaada wenu, mtakuwa wenye kuwashinda hawa makafiri.

التفاسير: