ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ಅಬ್ದುಲ್ಲಾ ಮುಹಮ್ಮದ್ ಮತ್ತು ನಾಸಿರ್ ಖಮೀಸ್

ಪುಟ ಸಂಖ್ಯೆ:close

external-link copy
70 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّمَن فِيٓ أَيۡدِيكُم مِّنَ ٱلۡأَسۡرَىٰٓ إِن يَعۡلَمِ ٱللَّهُ فِي قُلُوبِكُمۡ خَيۡرٗا يُؤۡتِكُمۡ خَيۡرٗا مِّمَّآ أُخِذَ مِنكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ewe Nabii, waambie mliowateka siku ya vita vya Badr, «Msisikitike juu ya fidia iliyochukuliwa kutoka kwenu. Iwapo Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Atajua kwamba kwenye nyoyo zenu pana wema, basi Atawapa kilicho bora zaidi kuliko mali yaliyochukuliwa kutoka kwenu, kwa kuwarahisishia nyinyi, kwa hisani Yake, wema mwingi - Mwenyezi Mungu Alitekeleza ahadi Yake kwa 'Abbas, Mwenyezi Mungu Awe radhi naye, na wengineo- na Atawasamehe madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha wa madhambi ya waja Wake wanapotubia, ni Mwenye huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
71 : 8

وَإِن يُرِيدُواْ خِيَانَتَكَ فَقَدۡ خَانُواْ ٱللَّهَ مِن قَبۡلُ فَأَمۡكَنَ مِنۡهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Na wakitaka kukwendea kinyume mara nyingine, wale uliowaacha huru miongoni mwa mateka, basi usikate tamaa. Kwani wao tangu hapo walikuwa wamefanya uhaini kwa Mwenyezi Mungu na wakakupiga vita., na Mwenyezi Mungu Akakupa ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani, ni Mwenye hekima katika kuendesha mambo ya waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 8

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَواْ وَّنَصَرُوٓاْ أُوْلَٰٓئِكَ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يُهَاجِرُواْ مَا لَكُم مِّن وَلَٰيَتِهِم مِّن شَيۡءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُواْۚ وَإِنِ ٱسۡتَنصَرُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ فَعَلَيۡكُمُ ٱلنَّصۡرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٞۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Hakika wale ambao wamemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakazifuata sheria Zake kivitendo, wakahama kwenda kwenye Nyumba ya Uislamu au nchi ambayo wataweza hapo kumuabudu Mola wao, wakapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali na nafsi, na Wale ambao waliowaweka Wahamiaji katika nyumba zao, wakawaliwaza kwa mali yao nawakaitetea dini ya Mwenyezi Mungu, hao ni wenye kusaidiana wao kwa wao. Ama wale walioamini na wasigure kutoka kwenye Nyumba ya ukafiri, basi nyinyi hamlazimishwi kuwahami na kuwatetea mpaka watakapogura. Na wakifanyiwa maonevu na Makafiri na wakataka msaada wenu, basi wakubalieni, isipokuwa iwapo ni dhidi ya watu ambao kuna makubaliano ya mkazo baina yenu na wao na hawajayavunja. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona matendo yenu, Atamlipa kila mtu kwa kadiri ya nia yake na tendo lake. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 8

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٍۚ إِلَّا تَفۡعَلُوهُ تَكُن فِتۡنَةٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَفَسَادٞ كَبِيرٞ

Na wale waliokanusha, ni wenye kusaidiana wao kwa wao. Na iwapo hamtakuwa, enyi Waumini, ni wenye kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, basi kutapatikana katika ardhi kufitiniwa Waumini na dini ya Mwenyezi Mungu na uharibifu mkubwa wa kuzuiwa njia ya Mwenyezi Mungu na kutiwa nguvu misingi ya ukafiri. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 8

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَواْ وَّنَصَرُوٓاْ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ حَقّٗاۚ لَّهُم مَّغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ

Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wakaacha majumba yao wakaelekea Nyumba ya Uislamu au kwenye nchi ambayo ndani yake watapata utulivu wa kumuabudu Mola wao, wakapigana jihadi kwa kulikuza neno la Mwenyezi Mungu, na wale waliowahami ndugu zao Muhājirūn, wakawapa Makao na wakawaliwaza kwa mali na kwa kuwapa nguvu. Hao basi ndio Waumini wakweli kidhati. Watapata msamaha wa madhambi yao na riziki njema iliyo kunjufu katika mabustani ya Pepo ya starehe. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 8

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۢ بَعۡدُ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ مَعَكُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ مِنكُمۡۚ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ

Na wale walioamini, baada ya hawa Muhājirūn na Anṣār, wakagura na wakapigana jihadi pamoja na nyinyi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hao ni katika nyinyi, enyi Waumini; wana haki mlizonazo nyinyi na wana majukumu mliyonayo. Na wenye ujamaa, kwenye hukumu ya Mwenyezi Mungu, baadhi yao wanapewa kipaumbele kwa wengine katika kurithiana kuliko Waislamu wa kawaida. Hakika Mwenyezi Mungu kwa kila kitu ni Mjuzi, Anayajua yanayowafaa waja Wake kuhusu kurithiana wao kwa wao kwa ujamaa na nasaba na kutorithiana kwa mapatano ya kujihami na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yale yaliyokuwa mwanzo wa Uislamu. info
التفاسير: