ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ಅಬ್ದುಲ್ಲಾ ಮುಹಮ್ಮದ್ ಮತ್ತು ನಾಸಿರ್ ಖಮೀಸ್

ಪುಟ ಸಂಖ್ಯೆ:close

external-link copy
3 : 5

حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةُ وَٱلدَّمُ وَلَحۡمُ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦ وَٱلۡمُنۡخَنِقَةُ وَٱلۡمَوۡقُوذَةُ وَٱلۡمُتَرَدِّيَةُ وَٱلنَّطِيحَةُ وَمَآ أَكَلَ ٱلسَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيۡتُمۡ وَمَا ذُبِحَ عَلَى ٱلنُّصُبِ وَأَن تَسۡتَقۡسِمُواْ بِٱلۡأَزۡلَٰمِۚ ذَٰلِكُمۡ فِسۡقٌۗ ٱلۡيَوۡمَ يَئِسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَٰمَ دِينٗاۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِي مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٖ لِّإِثۡمٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Mwenyezi Mungu Amewaharamishia mfu, naye ni mnyama aliyekufa mwenyewe bila ya kuchinjwa. Na pia Amewaharamishia nyinyi damu inayotiririka inayomwagwa, nyama ya nguruwe, mnyama ambaye wakati wa kuchinjwa ametajiwa jina lisilokuwa la Mwenyezi Mungu, mnyama aliyenyongwa kwa kuzibwa pumzi zake mpaka akafa, mnyama aliyekufa kwa kupigwa gongo au jiwe, mnyama aliyeanguka kutoka mahali pa juu au aliyeanguka kisimani akafa na mnyama aliyekufa kwa kupigwa pembe na mwenzake. Na pia Amewaharamishia mnyama aliyeliwa na mnyama mwingine kama simba, chuimarara, mbwamwitu na mfano wake. Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa za upungufu, Amewatoa, miongoni mwa wale Aliowaharamisha, kuanzia wale walionyongeka na waliofuatia, wale mliowahi kuwachinja kabla hawajafa, hao ni halali kwenu. Na Amewaharamishia nyinyi wanyama waliochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa vitu vilivyosimamishwa viabudiwe, viwe ni mawe au vinginevyo. Na Amewaharamishia kutaka kujua mambo, mliyoandikiwa na msiyoandikiwa, kwa viapo; navyo ni vipande ambavyo walikuwa wakitaka uamuzi kwavyo wakitaka kufanya jambo kabla hawajalifanya. Hayo mliyotajiwa katika aya hii kati ya yaliyoharamishwa, yakifanywa, huwa ni kutoka kwenye amri ya Mwenyezi Mungu na twaa Yake na kwenda kwenye maasia. Sasa imekatika tamaa ya makafiri kwamba nyinyi mtaiacha Dini yenu muende kwenye ushirikina baada ya mimi kuwapa ushindi juu yao. Basi msiwaogope wao na mniogope mimi. Leo nimeshawakamilishia dini yenu, Dini ya Uislamu, kwa kuuhakikisha ushindi na kuikamilisha Sheria, nimewatimizia neema zangu kwenu kwa kuwatoa kwenye giza la ujinga na kuwapeleka kwenye mwangaza wa Imani na nimewaridhia kwamba Uislamu ndio Dini, basi shikamaneni nayo wala msiiache. Na yule aliyepatikana na dharura ya njaa ikambidi ale mfu, na akawa hakukusudia kutenda kosa, basi inafaa kwake kumla. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumsamehe na ni Mwenye huruma naye. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 5

يَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَآ أُحِلَّ لَهُمۡۖ قُلۡ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَٰتُ وَمَا عَلَّمۡتُم مِّنَ ٱلۡجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ ٱللَّهُۖ فَكُلُواْ مِمَّآ أَمۡسَكۡنَ عَلَيۡكُمۡ وَٱذۡكُرُواْ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهِۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Wanakuuliza Maswahaba wako, ewe Nabii, «Ni kipi walichohalalishiwa kukila?» Waambie, «Mumehalalishiwa kula vilivyo vizuri na viwindwa vya wanyama mliowafundisha kati ya wanyama wanaowinda kwa kutumia makucha na meno yao, miongoni mwa mbwa, chui na kozi na kama hao kati ya wale wanaofundishwa. Mnawafundisha kuwatafutia viwindwa kwa yale Mwenyezi Mungu Aliyowafundisha. Basi kuleni wanyama waliowashikia na mlitaje jina la Mwenyezi Mungu wakati mnapowatuma kuwawindia. Na muogopeni Mwenyezi Mungu katika yale Aliyowaamrisha na yale Aliyowakataza.» Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 5

ٱلۡيَوۡمَ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَٰتُۖ وَطَعَامُ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ حِلّٞ لَّكُمۡ وَطَعَامُكُمۡ حِلّٞ لَّهُمۡۖ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ إِذَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحۡصِنِينَ غَيۡرَ مُسَٰفِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِيٓ أَخۡدَانٖۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلۡإِيمَٰنِ فَقَدۡ حَبِطَ عَمَلُهُۥ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na miongoni mwa ukamilifu wa neema ya Mwenyezi Mungu kwenu leo hii, enyi Waumini, ni kwamba Amewahalalishia vilivyo halali vizuri. Na vichinjwa vya Mayahudi na Wanaswara, iwapo watawachinja wanyama wao kuambatana na sheria yao, ni halali kwenu ; na vichinjwa vyenu ni halali kwao. Na Amewahalalishia nyinyi, enyi Waumini, kuwaoa wanawake wanaojihifadhi, nao ni wale walio huru kati ya wanawake Waumini wanaojizuia na uzinifu. Vilevile ni halali kuwaoa wanawake walio huru wanaojiepusha na uzinifu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, iwapo mtawapa mahari yao na mkawa mumejihifadhi kwa kutofanya uzinifu na kuweka mahawara na mkawa mumejiaminisha kuwa hamutaathirika na dini yao. Na mwenye kuzikataa sheria za fmani, basi vitendo vyake vimishaharibika, na yeye, Siku ya Kiyama, atakuwa ni miongoni mwa wenye kupata hasara. info
التفاسير: