ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
17 : 8

فَلَمۡ تَقۡتُلُوهُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُمۡۚ وَمَا رَمَيۡتَ إِذۡ رَمَيۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰ وَلِيُبۡلِيَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡهُ بَلَآءً حَسَنًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Kwa hivyo, hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua. Nawe hukutupa ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa, na ili awajaribu Waumini majaribio mazuri kutoka kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 8

ذَٰلِكُمۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُوهِنُ كَيۡدِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Hayo! Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha njama za makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 8

إِن تَسۡتَفۡتِحُواْ فَقَدۡ جَآءَكُمُ ٱلۡفَتۡحُۖ وَإِن تَنتَهُواْ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَإِن تَعُودُواْ نَعُدۡ وَلَن تُغۡنِيَ عَنكُمۡ فِئَتُكُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَوۡ كَثُرَتۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Mkiomba msaada wa ushindi, basi msaada wa ushindi ulikwisha wajia. Na mkikomeka, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkirejea, Sisi pia tutarejea. Na kundi lenu halitawanufaisha kitu hata kama yatakuwa mengi. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَأَنتُمۡ تَسۡمَعُونَ

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msigeuke mkamuacha hali ya kuwa mnasikia. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 8

وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ

ala msiwe kama wale wanaosema, "Tumesikia" na hali hawasikii. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 8

۞ إِنَّ شَرَّ ٱلدَّوَآبِّ عِندَ ٱللَّهِ ٱلصُّمُّ ٱلۡبُكۡمُ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡقِلُونَ

Hakika waovu mno wa wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale viziwi, na mabubu wasiotumia akili zao. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 8

وَلَوۡ عَلِمَ ٱللَّهُ فِيهِمۡ خَيۡرٗا لَّأَسۡمَعَهُمۡۖ وَلَوۡ أَسۡمَعَهُمۡ لَتَوَلَّواْ وَّهُم مُّعۡرِضُونَ

Na Mwenyezi Mungu angelijua heri yoyote ndani yao, angewasikilizisha, na lau angewasikilizisha, wangeligeuka hali ya kuwa wamepuuza. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 8

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَجِيبُواْ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمۡ لِمَا يُحۡيِيكُمۡۖ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يَحُولُ بَيۡنَ ٱلۡمَرۡءِ وَقَلۡبِهِۦ وَأَنَّهُۥٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Enyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaitia yale yenye kuwahuisha. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huizuia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye mtakusanywa. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 8

وَٱتَّقُواْ فِتۡنَةٗ لَّا تُصِيبَنَّ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنكُمۡ خَآصَّةٗۖ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Na jikingeni na mtihani ambao hautawasibu wale waliodhulumu pekee miongoni mwenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. info
التفاسير: