ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
95 : 6

۞ إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلۡحَبِّ وَٱلنَّوَىٰۖ يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَمُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتِ مِنَ ٱلۡحَيِّۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka na mbegu za tende, zikachipua. Humtoa aliye hai kutokana na maiti, na mwenye kumtoa maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnadanganywa? info
التفاسير:

external-link copy
96 : 6

فَالِقُ ٱلۡإِصۡبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيۡلَ سَكَنٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ حُسۡبَانٗاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ

Ndiye anayepambaza mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hesabu. Hayo ndiyo makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 6

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلنُّجُومَ لِتَهۡتَدُواْ بِهَا فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Na Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali ya bara na bahari. Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaojua. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 6

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ فَمُسۡتَقَرّٞ وَمُسۡتَوۡدَعٞۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَفۡقَهُونَ

Na Yeye ndiye aliyewazalishia kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanaofahamu. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 6

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ نَبَاتَ كُلِّ شَيۡءٖ فَأَخۡرَجۡنَا مِنۡهُ خَضِرٗا نُّخۡرِجُ مِنۡهُ حَبّٗا مُّتَرَاكِبٗا وَمِنَ ٱلنَّخۡلِ مِن طَلۡعِهَا قِنۡوَانٞ دَانِيَةٞ وَجَنَّٰتٖ مِّنۡ أَعۡنَابٖ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُشۡتَبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٍۗ ٱنظُرُوٓاْ إِلَىٰ ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَيَنۡعِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمۡ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Na Yeye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tukatoa mimea ya kila kitu. Na kutokana na baadhi yake tukatoa mimea ya kijani, tukatoa ndani yake punje zilizopandana; na kutokana na mitende katika makole yake yakatoka mashada yaliyo karibu; na mabustani ya mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapozaa na yakaiva. Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kaumu wanaoamini. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 6

وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ ٱلۡجِنَّ وَخَلَقَهُمۡۖ وَخَرَقُواْ لَهُۥ بَنِينَ وَبَنَٰتِۭ بِغَيۡرِ عِلۡمٖۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ

Lakini walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika, majini, ilhali Yeye ndiye aliyewaumba. Na wakamzulia kuwa ana wana wa kiume na wa kike, bila ya kuwa na elimu yoyote. Yeye Ametakasika, na ametukuka juu ya hayo wanayomsifu kwayo! info
التفاسير:

external-link copy
101 : 6

بَدِيعُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَمۡ تَكُن لَّهُۥ صَٰحِبَةٞۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيۡءٖۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Yeye ndiye Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Vipi awe na mwana, ilhali hakuwa na mke? Naye ndiye aliyeumba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua vyema kila kitu. info
التفاسير: