ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
33 : 25

وَلَا يَأۡتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَأَحۡسَنَ تَفۡسِيرًا

Wala hawatakuletea mfano wowote, isipokuwa na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 25

ٱلَّذِينَ يُحۡشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُوْلَٰٓئِكَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضَلُّ سَبِيلٗا

Wale ambao watakusanywa kwa nyuso zao hadi katika Jahannamu, hao watakuwa na mahali pabaya mno, nao ndio wenye kuipotea zaidi njia. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 25

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَا مَعَهُۥٓ أَخَاهُ هَٰرُونَ وَزِيرٗا

Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukamuweka pamoja naye kakaye, Harun, kuwa msaidizi. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 25

فَقُلۡنَا ٱذۡهَبَآ إِلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَدَمَّرۡنَٰهُمۡ تَدۡمِيرٗا

Tukawaambia: Nendeni kwa kaumu waliokanusha Ishara zetu. Basi tukawateketeza kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 25

وَقَوۡمَ نُوحٖ لَّمَّا كَذَّبُواْ ٱلرُّسُلَ أَغۡرَقۡنَٰهُمۡ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ لِلنَّاسِ ءَايَةٗۖ وَأَعۡتَدۡنَا لِلظَّٰلِمِينَ عَذَابًا أَلِيمٗا

Na kaumu ya Nuhu, walipowakanusha Mitume, tuliwazamisha, na tukawafanya ni Ishara kwa watu. Na tumewaandalia madhalimu adhabu chungu. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 25

وَعَادٗا وَثَمُودَاْ وَأَصۡحَٰبَ ٱلرَّسِّ وَقُرُونَۢا بَيۡنَ ذَٰلِكَ كَثِيرٗا

Na (tuliwaangamiza) kina 'Adi na Thamudi na watu wa Rass na vizazi vingi vilivyokuwa kati yao. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 25

وَكُلّٗا ضَرَبۡنَا لَهُ ٱلۡأَمۡثَٰلَۖ وَكُلّٗا تَبَّرۡنَا تَتۡبِيرٗا

Na wote tuliwapigia mifano, na wote tuliwaangamiza kabisa kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 25

وَلَقَدۡ أَتَوۡاْ عَلَى ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِيٓ أُمۡطِرَتۡ مَطَرَ ٱلسَّوۡءِۚ أَفَلَمۡ يَكُونُواْ يَرَوۡنَهَاۚ بَلۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ نُشُورٗا

Na kwa yakini wao walikwisha ujia mji ulioteremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiuona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 25

وَإِذَا رَأَوۡكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا ٱلَّذِي بَعَثَ ٱللَّهُ رَسُولًا

Na wanapokuona, hawakuchukulii isipokuwa ni mzaha tu, na (wanasema): Ati huyu ndiye Mwenyezi Mungu alimtuma kuwa Mtume? info
التفاسير:

external-link copy
42 : 25

إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنۡ ءَالِهَتِنَا لَوۡلَآ أَن صَبَرۡنَا عَلَيۡهَاۚ وَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ حِينَ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ مَنۡ أَضَلُّ سَبِيلًا

Kwa hakika alikuwa karibu zaidi kutupoteza tuiache miungu yetu, lau kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapoiona adhabu, ni nani aliyepotea zaidi njia. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 25

أَرَءَيۡتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيۡهِ وَكِيلًا

Je, umemwona aliyeyafanya matamanio yake kuwa ndiyo mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake? info
التفاسير: