ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
29 : 13

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ طُوبَىٰ لَهُمۡ وَحُسۡنُ مَـَٔابٖ

Wale walioamini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 13

كَذَٰلِكَ أَرۡسَلۡنَٰكَ فِيٓ أُمَّةٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهَآ أُمَمٞ لِّتَتۡلُوَاْ عَلَيۡهِمُ ٱلَّذِيٓ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ وَهُمۡ يَكۡفُرُونَ بِٱلرَّحۡمَٰنِۚ قُلۡ هُوَ رَبِّي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ مَتَابِ

Ndivyo hivyo tulivyokutuma kwa umma ambao wamekwsiha pita kabla yao umma nyingine, ili uwasomee yale tuliyokufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani (Mwingi wa Rehema)! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndiyo marejeo! info
التفاسير:

external-link copy
31 : 13

وَلَوۡ أَنَّ قُرۡءَانٗا سُيِّرَتۡ بِهِ ٱلۡجِبَالُ أَوۡ قُطِّعَتۡ بِهِ ٱلۡأَرۡضُ أَوۡ كُلِّمَ بِهِ ٱلۡمَوۡتَىٰۗ بَل لِّلَّهِ ٱلۡأَمۡرُ جَمِيعًاۗ أَفَلَمۡ يَاْيۡـَٔسِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن لَّوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَهَدَى ٱلنَّاسَ جَمِيعٗاۗ وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُواْ قَارِعَةٌ أَوۡ تَحُلُّ قَرِيبٗا مِّن دَارِهِمۡ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ وَعۡدُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ

Na kama ingelikuwako Qur-ani inayoendeshewa milima, na kupasuliwa kwayo ardhi, na kusemeshwa kwayo wafu, (basi ingelikuwa Qur-ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa bila ya shaka angeliwaongoa watu wote? Na wale waliokufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa yale waliyoyatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 13

وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَأَمۡلَيۡتُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ ثُمَّ أَخَذۡتُهُمۡۖ فَكَيۡفَ كَانَ عِقَابِ

Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako. Na nikawapururia wale waliokufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu! info
التفاسير:

external-link copy
33 : 13

أَفَمَنۡ هُوَ قَآئِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡۗ وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ قُلۡ سَمُّوهُمۡۚ أَمۡ تُنَبِّـُٔونَهُۥ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَم بِظَٰهِرٖ مِّنَ ٱلۡقَوۡلِۗ بَلۡ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ مَكۡرُهُمۡ وَصُدُّواْ عَنِ ٱلسَّبِيلِۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ

Je, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndiyo mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi, au ni maneno matupu tu? Bali wale waliokufuru wamepambiwa njama zao na wamezuiliwa njia ya sawasawa. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana wa kumwongoa yeyote. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 13

لَّهُمۡ عَذَابٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَشَقُّۖ وَمَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٖ

Wana adhabu katika uhai wa dunia, na adhabu ya Akhera hakuna shaka ndiyo ngumu zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu. info
التفاسير: