ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
104 : 12

وَمَا تَسۡـَٔلُهُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote. info
التفاسير:

external-link copy
105 : 12

وَكَأَيِّن مِّنۡ ءَايَةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يَمُرُّونَ عَلَيۡهَا وَهُمۡ عَنۡهَا مُعۡرِضُونَ

Na ni ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia, lakini wao wanazipuuza. info
التفاسير:

external-link copy
106 : 12

وَمَا يُؤۡمِنُ أَكۡثَرُهُم بِٱللَّهِ إِلَّا وَهُم مُّشۡرِكُونَ

Na wengi wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina. info
التفاسير:

external-link copy
107 : 12

أَفَأَمِنُوٓاْ أَن تَأۡتِيَهُمۡ غَٰشِيَةٞ مِّنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ أَوۡ تَأۡتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ

Je, wana amani kuwa iwajie adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au iwajie Saa ya Qiyama kwa ghafla, na hali hawatambui? info
التفاسير:

external-link copy
108 : 12

قُلۡ هَٰذِهِۦ سَبِيلِيٓ أَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِيۖ وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa ufahamu mzuri - mimi na wale wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina. info
التفاسير:

external-link copy
109 : 12

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰٓۗ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۗ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je, hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo bora kwa wamchao Mungu. Basi hamtumii akili? info
التفاسير:

external-link copy
110 : 12

حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسۡتَيۡـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ كُذِبُواْ جَآءَهُمۡ نَصۡرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَآءُۖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُنَا عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Hata Mitume walipokata tamaa (ya watu wao kuamini) na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, kwa hivyo wakaokolewa sawasawa tuwatakao. Na adhabu yetu haiwezi kurudishwa dhidi ya kaumu wahalifu. info
التفاسير:

external-link copy
111 : 12

لَقَدۡ كَانَ فِي قَصَصِهِمۡ عِبۡرَةٞ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِۗ مَا كَانَ حَدِيثٗا يُفۡتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Hazikuwa hadithi tu zilizozuliwa, bali ni za kusadikisha yale yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kina wa kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu inayoamini. info
التفاسير: