ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
98 : 11

يَقۡدُمُ قَوۡمَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَأَوۡرَدَهُمُ ٱلنَّارَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡوِرۡدُ ٱلۡمَوۡرُودُ

Siku ya Qiyama atawatangulia kaumu yake na atawaingiza Motoni. Na muingio mbaya zaidi ulioje huo unaoingiwa! info
التفاسير:

external-link copy
99 : 11

وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِۦ لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ بِئۡسَ ٱلرِّفۡدُ ٱلۡمَرۡفُودُ

Nao walifuatishwa laana hapa (duniani) na Siku ya Qiyama. Ni kipawa kibaya zaidi kilichoje walichopewa! info
التفاسير:

external-link copy
100 : 11

ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّهُۥ عَلَيۡكَۖ مِنۡهَا قَآئِمٞ وَحَصِيدٞ

Hizi ni katika habari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine ilifyekwa. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 11

وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡۖ فَمَآ أَغۡنَتۡ عَنۡهُمۡ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِي يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ لَّمَّا جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَمَا زَادُوهُمۡ غَيۡرَ تَتۡبِيبٖ

Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao. Na miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia isipokuwa maangamio tu. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 11

وَكَذَٰلِكَ أَخۡذُ رَبِّكَ إِذَآ أَخَذَ ٱلۡقُرَىٰ وَهِيَ ظَٰلِمَةٌۚ إِنَّ أَخۡذَهُۥٓ أَلِيمٞ شَدِيدٌ

Na hivyo ndivyo ulivyo mshiko wa Mola wako Mlezi anapoishika miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mshiko wake ni mchungu na mkali. info
التفاسير:

external-link copy
103 : 11

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّمَنۡ خَافَ عَذَابَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّجۡمُوعٞ لَّهُ ٱلنَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّشۡهُودٞ

Hakika katika hayo ipo ishara kwa yule anayehofu adhabu ya Akhera. Hiyo ndiyo Siku itakayokusanyiwa watu, na hiyo ndiyo Siku itakayoshuhudiwa info
التفاسير:

external-link copy
104 : 11

وَمَا نُؤَخِّرُهُۥٓ إِلَّا لِأَجَلٖ مَّعۡدُودٖ

Na wala hatuiahirishi isipokuwa kwa muda unaohisabiwa. info
التفاسير:

external-link copy
105 : 11

يَوۡمَ يَأۡتِ لَا تَكَلَّمُ نَفۡسٌ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ فَمِنۡهُمۡ شَقِيّٞ وَسَعِيدٞ

Siku hiyo itakapokuja, nafsi yoyote haizungumza isipokuwa kwa idhini yake. Basi miongoni mwao watakuwamo waliomo mashakani na wenye furaha. info
التفاسير:

external-link copy
106 : 11

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ شَقُواْ فَفِي ٱلنَّارِ لَهُمۡ فِيهَا زَفِيرٞ وَشَهِيقٌ

Ama wale wale walijitia mashakani, hao watakuwa Motoni, humo watavuta pumzi na kuitoa kwa ugumu mkubwa. info
التفاسير:

external-link copy
107 : 11

خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ

Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda atakavyo. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 11

۞ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ سُعِدُواْ فَفِي ٱلۡجَنَّةِ خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۖ عَطَآءً غَيۡرَ مَجۡذُوذٖ

Na ama wale waliofurahishwa, wao watakuwa katika Pepo wakidumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisicho na kikomo. info
التفاسير: