[1] Mola Mlezi ni yule anayewalea walimwengu wote. Nao walimwengu ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu. Na ulezi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa viumbe wake ni wa aina mbili: Wa kiujumla na wa mahususi. Ama wa kiujumla ni kuumba kwake viumbe, kuwapa riziki, na kuwaongoza katika yale yaliyo na masilahi yao. Nao ulezi wake mahususi ni kulea kwake vipenzi wake kwa imani, na kuwawezesha kuifikia, na kuwakamilishia imani hiyo. (Tafsir Assa'dii)